Taarifa ya Uongozi wa JF umeleta tumaini jipya

Sipendi huo msemo usiokuwa na time limit wazee! “eti mapema kadri iwezekanavyo” kuna siku au tarehe inaitwa hivyo! au ndio kutaka kutupa matumaini yasiyo na mwisho’ wao wapamane tu wakishamalizana na hao wakoloni pori wafungue forum’ sisi hatuna shida tupo zetu kenyatalk tunaendelea kupiga soga’ tena huku tuko salama zaidi’ hakuna wa kututisha, yaani Jforum hata wakirudi kwa mashariti waliyopewa ya kuexpose watu kwa tcra nani ajiingize kichwa kichwa. heh! sisi tunaaki huku huku wazee mpaka watuhakikishie usalama wetu. kule tutakuwa kwenye jukwaa la mapenzi na kubet

Kwani iko mbali basi!, hii hapa:
www.bongoforums.com

Hii hapa mkuu:
www.bongoforums.com

Real talk…haraka iwezekanavyo ni lini??..baada ya muda mfupi ni lini??..ni bora wakaka kimya huku wakiendelea kutatua tatizo…btw kenya talk na penyewe sio haba

Hizi forums zitakazoanzishwa tz siyo za kuamini sana, yaweza kuwa tego

huko haturudi na tunabaki huku huku,huko bongo kuna vitisho sana,hakuna uhuru wa kujieleza hatukubali tunabaki hukuhuku

Mkuu kwa huku Africa muda mfupi ujao haupungui miezi 6!

kenyatalk Mungu awabariki tunashukuru kwa fulsa hii; endeleeni kutushirikisha.

tupo kitambo…wewe ndo mgeni. hizi ndo ID zangu JF na hapa nipo kitambo (miss natafuta, shunie, etc)

new villager = new member, senior villager = senior member, etc

sawa…

Warudi hewani kwani wametoka hewani?

Hiyo in misemo tu kama vile katika lugha ya kigeni wanavyosema Off the Air, maana yake no kuwa hawapo hewani au mtambo umezimwa…

Nilisoma taarifa ya Mara tu baada ya kuzimwa JF ambayo ilisema kuwa kwa wale watumiaji was JF walioko nje ya nchi, huduma hiyo itarudi mapema, lakini kwa wale walioko TZ Huduma hiyo itategemea jinsi Uongozi wa JF utakavyochakarika…

Lakini katika taarifa waliyotoa siku 2 zilizopita ndipo wanaposema kuwa JF inatarajia kurejea Very Soon…

Lakini hawajasema hiyo Very Soon ni lini?

Hawajasema Mkuu.
Ukiona wanasikilizia sana ujue wametishwa, kama suala ni kodi na vibali, hela siyo tatizo, wangelipia haraka na JF ingerudi hewani haraka. Ukimya huu siyo wa kodi wala vibali.

Kurudi kwa jf ni kukubali privacy isiwepo

That’s true

Na kwa jinsi Magufuli anavyojifananisha na Mungu, hataki kukosolewa kabisa huyo Ngosha

Na ni kweli kabisa ya kuwa kwa Maxence Melo, pesa zilizotakiwa kilipwa na TCRA wangeweza kabisa kuzilipa

Ila najua kuchelewa kurudi kwao watakuwa wanashindana kwenye kuweka privacy ya watumiaji wa JF

Na hii ndo itafanya jf Ife kibudu!!Magu threats yake kubwa ni Jf na ndo iymt was his target so ameachieve kiasi chake

Ni bora sisi tumejitafutia ukimbizi huku Kenyatalk…

Tena hili jukwaa liko poa sana, halina kupigana ban kienyeji enyeji tu

Nakumbuka sana aliposema anatamani Malaika washuke duniani kuizima mitandao ya kijamii…

Na target yake iwapo hao “malaika” wake wangeshuka ilikuwa namba moja in JF

Kwa hiyo hats kama JF itafunguliwa ni lazima turudi kimagutu magutu, ama sivyo atakula vichwa vyetu huyu Magu