Swali La Uzalendo Kwa Wana JF, Ukimbizini na Ugenini, Jee Tuanike Tuu Dirty Linen Zetu Kibarazani?, Au Uani Ili Kuhifadhi Aibu Yake, Aibu Yetu?.

Wanabodi wote wa ukimbizini ugenini,

Salaam.

Nina swali dogo kuhusu uzalendo wa ukimbizini na ugenini.
Inapotokea, baba yako akiwa mlevi, karudi, kajitapikia sebuleni na kampiga mama kwa kisa mama kamwita mlevi, na ulipoamka asubuhi ukawasikia baba na mama wanazozana chumbani kuwa saiti, mama akigomba, kwa kwa nini ujikolee kitandani?, hatuna mtoto mdogo, tukianika godoro nje, majirani watatuonaje?, wewe mtoto ulishuhudia baba akijitapikia, ulisikia baba akiitwa mlevi na kushuhudia kipigo kwa mama, kesho yake asubuhi ukashuhudia godoro likitolewa kuanikwa uwani, wewe unapokwenda shule. huko barabarani na mitaani jee utahadithia tuu kuwa baba ni mlevi na jana kajitapikia, kampiga mama, na usiku kajikojolea kitandani?!, au utajinyamazia kwa kusikitika, kuhuzunika na kutahayari kwa hali ya nyumbani, kuficha aibu ya baba na matezo ya mama?.

Mambo mengine ni aibu, tuyaache na kuyahifadhi kama siri za ndani, ikibidi kumsitiri baba yetu, japo kweli ni mlevi, lakini kwa huku nje, ugenini, tumsitiri kisha nyumbani ndipo tubanane nae ili majirani wasijue aibu za baba yako, na mateso ya mama yako?.

Uzalendo wa kweli wa nchi yako jee sio ni pamoja na kuficha siri zetu za ndani?.
Jee kwa jinsi watu wanavyomtukana Baba nwenye nyumba huku ugenini, japo ni kweli, lakini ni haki kweli?, ni uzalendo?.

Paskali

Kwanza sikutegemea na wewe utakuja huku baada ya likizo uliyojipa kule JF, Huku tutaendelea kuanika magodoro na chupi zetu maana haya amejitakia mwenyewe chafu barazani. Baba akiwa mlevi hiyo ni aibu yake yeye binafsi hainigusi mm. kwa hatua tuliyofikia ni bora zigo la lawama limwendee baba peke yake

nikajua utakuwa new villager

paskali kwanza pole kwa mkwala uliopitia, lkn kumsema baba kwa jirani inaweza kuwa dawa ya yy kutorudia madhambi yake,ona katuziba midomo sasa tunasemea wapi? kwa hiyo anafanya haya makusudi siyo? kwa kuwa anauwezo wa kuita malaika wafunge mitandao siyo ila anaudhi sana ila basi tu.

Mkuu @Pascal Mayalla ni furaha kubwa kukuona hapa…

Hakuna jinsi kwa huyu Baba…

Lazima ukweli usemwe tu…

La muhimu yote anayosemwa nayo yawe KWELI.

Ni siku za karibuni tu tuliwazika wapendwa wetu Maria na Consolata,mapacha walioungana. Wailukwa walemavu. Tulishauriwa tusiwafiche walemavu ndani,tuwatoe kwenye jamii ili kwa pamoja tushirikiane kuwahudumia.

HAKUNA WAKATI MZURI WA KUMPIGA NYOKA KICHWANI KAMA HUU.

Huku ndio mahali pazuri kwa kuweka udhalimu wote hadharani. Hata huko nyumbani tulikuwa tunatumia online platforms ambazo zinaonekana dunia nzima. Cha muhimu ni kusema ukweli.

Sijao

Niliposoma kichwa cha habari nikaona nisiendelee na jibu lake ni kama ifuatavyo

Baba akizidi kuwa muhuni ndani ya familia sometimes hata kichapo aweza kupata…usinihoji kuhusu hili…Biblia imeandika Enyi wazazi msiwachokoze watoto wenu…
Maana ya Neno hili ni kwamba, watoto ni wanadamu na wananyama kama Baba na wahisi maumivu yoyote watendewayo…
Kifupi nikwamba huu sio mda tena wakumbembeleza JIWE…kama mbaya wacha iwe mbaya.
Binafsi sitasubiri mboga ifike mezani nitamwaga.

Yote yawekwe bayana mradi tu yawe ya kweli.

acha baba asulubiwe, watoto hawana maji safi wala madawa yeye ananunua SUV la bei mbaya ili akajitape bar mbele ya walevi wenzake. alafu bila aibu anajitapa mbele yetu “fahari ya familia ni SUV”

mkuu sijui nimefanyaje naona comment yangu ipo ndani ya bandiko lako

Acha watu tumsasambue Magufool tupendavyo. Haaaaahaaaaa.

Huyu jiwe anastahili kuzomewa sana vinginevyo atavimba kichwa kwa kupenda sifa!

Tatizo ni kuwa baba huyu mlevi anajikojolea hadharani huku kila mtu akimshuhudia, sasa utamfichia vipi aibu yake?

Mlevi ni mlevi tu siri yake haifichiki

Hmm!.. Nadhani muda utasema zaidi…

mayalla NI wewe kweli?

Kama uani kuna nafasi ya kuanikia kwa nini uanike barazani?, tena ugenini?. Kwa kuanika barazani ugenini, huoni kama ni kujiaibisha?.
P.

Ni mimi na hapa simzungumzii mtu yoyote real bali nimetoa tuu hypothetical scenario ya siri za ndani za aibu kuzitoa nje tena ugenini!.

P.