Matiangi used to be the first name to come up but recently his image has been tainted by his past deed of disobaying court orders and River Yala bodies, so this begs the question, WHO CAN AKE ON JSKS IN 2027?
MORARA & KASMUEL can make good running mate for a candidate such as Omtata
Kwanza pendeni nchi yenu na vyote vinavyoihusu nchi yenyewe, ikiweko pia kuwapenda wananchi wenzenu, wawe wezi ama makasisi, ili mapatano yapatikane. Ikubalike kwa kila mmoja kuwa hakuna aliye mwema kuliko mwenzake.
Pili, mbadilishe katiba. Maradhi ya nchi yenu yanatokana na hii katiba yenu mbovu na yatatibiwa kwa kuikarabati kwa kiasi kikubwa ama kuibadilisha yote kabisa!
Tatu, ifahamike kwamba Kenya hamna “mkubwa” anayeweza kunguruma akasikika kama vile Magufuli ama Kagame. Mnawadharau wenzenu wanaojitokeza kuwaongoza hata kuzikosea heshima idara na ofisi zenu mahsusi zinazokaliwa na hao mnaowachukia. Kubalini kwamba hamuwezi kuwa wakubwa nyote pamoja kwa wakati mmoja. Aliyeibuka kama kiongozi, awe wa nyumba kumi, mzee wa mtaa, chifu, rais…, kiongozi awaye yeyote awezeshwe na kupewa nguvu na nyinyi wananchi na katiba yenu madhubuti. Mnapowatukana na kuwavamia manyumbani kwao kwa sababu mmewashuku kwa hili ama lile mnawavunja moyo na hawatafanya kazi yenu sawasawa.
Nne, fanyeni makadirio ya mpaka hapo mlipofikia mwoone mafanakio ama hasara gani mmepata kwa kufanya mambo yenu vile mnavyofanya ili mjue ni kwa njia gani kila mmoja wenu atabadilika kibinafsi. Chukia anayeita maandamano na uharibifu wa mali na biashara za umma kama unavyowachukia wanaojihusisa na kufanya ufisadi. Unapojipata kwenye hatamu za uongozi usiibe, na sisi tusikushuku bila sababu. Tujiwekee jukumu kwamba sote tunataka nchi iendelee. Tusieneze uongo kuwahujumu wenzetu. Tukatae kudanganywa na kasisi kama tunavyokataa kudanganywa na jambazi. Haki itembee.