Nimeboeka kwa hao nikaona nitoke kidogo majioni niende nitembee. Kufika grao nikapata watoto around 19yrs 20yrs hadi 22yrs wanacheza futa. Bado ilikuwa hii ya mtaani si official.
Nikaamua kujoin ata mimi nipunguze uzee nisiwe mnono kama @Yuletapeli. Nakwambia hao vijana wa ghetto wameivia ball kwa epl superstars.
Nilipigwa machobo zikifuatana kali kali nikaamua kuwa serious ati nachase bolingo nakuambia nimepigwa makanzu zangu tamu.
Saa hio vijana wanacheka cheka wakinipasha nilipigwa ingine safi huyo kijana akavuta tracksuit yangu chini nikabaki na boxer.
Haidhuru acha niingie winger ball za juu ama chini zikikuja ni control dribble kiasi,pass ama shot to score. Nilipata Defender mmoja mluhya amekula vizuri. Tulikuwa tunachase ball pamoja then nikaona ni kama nimemshinda pace. But it was a trap.
Alinipiga body ingine mwecheche nikaloose control na kuanguka na huko hivyo nikiwa chini naona wasee wamenicheka ata si ile ya kucheka ni kuniaibisha tu.
Nikaingia keeper nikajiona Raya then nilikuwa nasave shots mob sana but after sometime it was then i noticed hizo shots zilikuwa za kuniumiza and not to score. Nilichukua tu vitu zangu na kuenda Airport it seems i am good at horizontal engineering.