Sitosahau safari yangu toka Tanzania mpaka Kenya.

Tukiwa kwenye basi kuukuu lilochakaa lenye viraka vingi vilivyoungwa bila kuzingatia ustadi na uweledi wa taaruma huku tukiwa tumebanana mithiri ya ndizi kwenye mkungu ulio kubali mbolea ya asili. Kuna Abiria waliojikatia tamaa na safari ya basi hili kutokana na majibu ya kuudhi ya wasaidizi wa busi hili, Abiria kwenye hili basi hawaishi kelele zinazoonyesha machungu na huzuni mioyoni mwao lakini hawana wa kumwelezea shida yao, Wapo waliojaribu kumuhusia Dereva mwendo na mwenendo wa safari kuwa ni mbaya lakini wasaidizi wa busi hili hawakusita kutumia nafasizao ndani ya busi kumkingia kifua Dereva wa busi dhidi ya mwendo wake mbaya unaozidi kulichakaza basi hili,
Basi linalopumua kwa kutumia tundu moja huku matundu mengine yakiwa yamezibwa na wahudumu wa busi hili ili waweze kupata hewa safi bila kujari wasafiri wengine wengine.
Kutokana na ukosefu wa elimu yenye tija na kujivikaubabe Dereva, Makondakta na watumishi wengine ijapo kuwa wana taaruma Zao ila wamekuwa watumwa wa matumbo yao kwenye busi wanajisikia tu kujichukulia nauli kwa wasafiri kiasi chochote wanachotaka huku wakiwatishia kua wataikatisha safari Yao wasipo kubali.
Bila kujali nini wanahitaji wasafiri Mara anatokea muhudumu wa busi hili akitoa tamko ni ruhusa kutumia simu bila internet kwa Abiria na pia ni marufuku kutumia simu yenye internet uwepo ndani ya basi maana unamchanganya dereva pindi aongozapo basi.
Baada ya kukumbana na ghasia nyingi sana ndani ya basi ikanibidi Mimi na baadhi ya Abiria tutafute basi jingine kwa ajili ya kuhakikisha tunafika salama safari yetu.
Mpaka. muda huu. busi la Kenya limetupatia Msaada. ili. kuikamilisha. safari
Nawasilisha.

Mkuu Ndio hili tulilopanda Au

Ndo hili hili si unajua tumekuja Abiria kwa mafungu wengi ila nasikia wengimefaulisha kwenye sijui nini forums ordinary maana sitaki hata kuijua sababu Huduma Zao mbaya.

Ndugu yangu wale waliofaulishwa Kwenye lile jipya usalama Wao utakua shakani Kwani Inawezekana linamilikiwa na lile genge la mzee Baba kipara

Time will tell…

Cc: @Mahondaw

Safari bila nauli hii

msafiri kafiri