Shairi(poem) - Nyoka

[FONT=Courier New][SIZE=6](Vionjo vya mashairi ya Tanzania)

Nyumba umeshaijenga, Gharama ukatumia,
Hukutaka wa kupanga, Mwenyewe ukaingia
Milango ukaifunga, Ulinzi ukatimia
Nyoka kaingia ndani, Utafanya nini sasa?

Utaanza kutafuta, Wapi ameingilia?
Utaanza kutafuta, Mtu wa kukuvunjia?
Utaanza kujifuta, Ili sasa kukimbia?
Nyoka kaingia ndani, Utafanya nini sasa?

Ni nyoka mwenye milia, Tena anaogopeka
Nyoka asiye tulia, Kila kitu anataka
Unga anautumia, Bila hata ya kupika
Nyoka kaingia ndani, Utafanya nini sasa?

Ameshaanza kutaga, Ili kupata wengine
Utaanza kumfuga, Awe na miraba nane?
Yeye hapo anapanga, Aje ili mpambane
Nyoka kaingia ndani, Utafanya nini sasa?

Ndugu yangu huyo swila, Wengi ameshaumiza
Zetu hazijui mila, Anapenda kingereza
Yeye anapenda kula, wenzake kuwaumiza
Nyoka kaingia ndani, Utafanya nini sasa?

Utamwita Seremala, Aje aivunje nyumba?
Joka ndani limelala, Macho bila ya kufumba
Lataka kujitawala, Kuvamia kwenye chumba
Nyoka kaingia ndani, Utafanya nini sasa?

Dawa yake pilipili, Ichome utamuweza
Bila hata kujadili, Lazima kuangamiza
Maana ana sumu kali, Lazima kutokomeza
Dawa ya nyoka moja tu, Ni kuchoma pilipili

Rungu umepewa Kweli, Inabidi litumie
Nguvu yako ni kamili, Fanya kazi atimue
Umkate mapingili, Na kisha aangamie
Dawa ya nyoka moja tu, Ni kuchoma pilipili

Fukunyua fukunyua, Mayai kuteketeza
Pangua panga pangua, Nyumba yako kupendeza
Mianya yote zibua, Uozo kutokomeza
Dawa ya nyoka moja tu, Ni kuchoma pilipili

Kelele hizo kilio, Nyoka amepigwa nyundo
Wewe ziba masikio, Tena na ukaze mwendo
Hilo hapo ni fagio, Litaondoa uvundo
Nyoka sasa amelewa, Ni kuponda ponda kichwa[/SIZE][/FONT]

Maghufool anafunga Jamii forums lini.

https://www.jamiiforums.com/
Check if exists

wanafunzi wako shule wewe uko wapi

This Swahili hurts my eyes to read.

[ATTACH=full]149492[/ATTACH]

hongera mdau, shairi tamu sana

:smiley:

:smiley: