SERIKALI MFU NI SERIKALI INAYODHANI INA NGUVU ZAIDI YA WANANCHI WAKE

Hili ni tatizo kubwa sana kwenye nchi zetu za Afrika. Mara nyingi viongozi wa kiafrika wametawaliwa na hulka ya ujuaji pasipo kushaurika, hii hupelekea viongozi hawa kuwa na dharau kwa wananchi waliowaweka madarakani. Viongozi hawa huwa na kauli tata zenye kukatisha tamaa wananchi ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kubwa kulazimisha hoja sao ziwafikie wananchi.
Kutokana na dhana hii ya kutumia nguvu ya hoja , inasababisha maendeleo kudumaa kwenye nchi nyingi za afrika. Hii ni ukweli kwamba hata watumishi wa uma ambao wamepewa dhamana na kufanya uzalishaji wa huduma na bidhaa -kukata tamaa na kufanya ndivyo sivyo.
Nchi ambayo huduma za jamii zinatolewa ndivyo sivyo ni nchi yenye serikali mfu.
Viashiria vya serikali mfu
-Dola kutumika kukandamiza wananchi
-Kuminya uhuru wa habari
-Kiongozi wa nchi kuamini ana busara na maarifa kuliko yeyote

Funguka kabisa usiogope… ngoja nikusaidie kidogo:
Serikali mfu zinaongozwa na watu mfu, wasio na uhalali kisheria kuwa viongozi. Mfano mzuri ni Maghufuli. Mnafahamu lichama lake lilipindua matakwa ya wananchi kwa kufoji matokeo ya uchaguzi mchana kweupe. Majitu kama haya definitely yanakuwa yamepanic tokea awali… kwa hiyo ni vigumu kutegemea chochote cha maana kutoka kwayo. Cha msingi wananchi tujifanyie yetu… maana haya ma viongozi mfu yako radhi kuuwa watu… tena bila aibu. Rejea kisa cha TLS…

Tutazidi kukandamizwa hadi tuwe kama chapati…wachagua hovyo uishia kuongozwa hovyo…labda tuibebe ile nchi kichwani tuitumbukize bahari…kila kilichomo kiteketee

Eeeeeee mwenyezi Mungu utunusuru na dhahama hii.

Funguka mkui

Serikali yangu sio mfu iko hai

Udhaifu wetu ndiyo nguvu na furaha kwao…

Hahahahahaha lol mkuu umetisha dikteta

Kiukweli HAKUSHINDA.

tatizo la viongozi wa-Afrika wanafikiri wao ndo wanamonopoly of
1.Knowledge
2.Truth
3.Wisdom

!
!
Maamae Teknolojia Ipo Mbele Ya Sheria. Bado Tupoooo