Sakata la Lugumi: Kwanini miaka miwili baadaye?

Kwanini huyu dikteta alifufue sakata la Lugumi miaka miwili baadaye? Je, atashinikiza na uchunguzi wa upotevu wa trillion 1.5 ufanyike na Tume huru? Je, atashinikiza na uchunguzi wa waliotoa rushwa ili kununua Wabunge wa upinzani?

Hii habari ni ya May 20, 2016

Wakati sakata la kampuni ya LUGUMI Enterprises likiendelea kutikisa nchi, mashine za utambuzi wa alama za vidole, zimeanza kufungwa katika mikoa kadhaa ikiwamo ya Dodoma na Geita.

Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kwamba juzi mashine hizo zilifungwa katika vituo vya polisi vya wilaya za Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma na kazi hiyo ilitarajiwa kufanywa mjini Dodoma jana. Pia, vyanzo vya habari kutoka mkoani Geita vimeithibitishia Mwananchi kwamba mashine hizo zimefungwa katika vituo vitano vya polisi.

Kampuni ya LUGUMI iliingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011 kufunga mashine hizo kwenye vituo 108, lakini hadi wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anamaliza ukaguzi, ni vituo 14 tu vilikuwa vimefungwa mashine hizo.

Taarifa hiyo ya CAG ililistua Bunge na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) iliunda kamati ndogo ili kuzunguka mikoani kuthibitisha taarifa hiyo ya mkaguzi mkuu.

Lakini wakati kamati hiyo ikiwa imepewa kazi hiyo, Mwananchi imeambiwa kuwa mashine hizo zinafungwa.

“Tulikuwa na LUGUMI hapa,” alisema mmoja wa watoa habari waliozungumza na Mwananchi.

“Vijana wa LUGUMI walikuwa wanafunga mashine, wameondoka kwenda Kongwa. Kesho (jana) watakuwa Dodoma.”

Imeelezwa kuwa vijana wanaofunga mashine hizo walikwenda Mpwapwa wakitokea Kibaha mkoani Pwani. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, katika Mkoa wa Geita, mashine hizo zimefungwa wilaya za Nyang’hwale, Chato, Geita, Bukombe na Mbogwe.

Alipotafutwa kutoa ufafanuzi wa kazi ya ufungaji mashine hizo, Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Latson Mponjoli alisema suala hilo ni la kitaifa hivyo kutaka watafutwe viongozi wa kitaifa.

“Mimi nitazungumzia nini kuhusiana na LUGUMI? Suala hilo ni la kitaifa unaniuliza mimi? Hilo suala mtafute waziri mwenye dhamana au IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) ndiyo wenye mamlaka ya kulizungumzia jambo hilo,” alisema Kamanda Mponjoli.

Lakini juhudi za kumpata IGP Ernest Mangu kwa simu hazikufanikiwa badala yake simu yake ilipokewa na msaidizi wake. Mwandishi alipoanza kuzungumza naye, simu yake ilikatika.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga alisema hataki kujibu maswali yanayohusu kampuni hiyo na kwamba mwandishi awasiliane na kampuni hiyo. “Taarifa za LUGUMI kawaulizeni LUGUMI wenyewe, sipendi kujibu maswali ya kijinga na upumbavu, kwa sababu nimekwenda vituoni mwenyewe nimejionea,” alisema na kukata simu. Alipopigiwa simu tena ili aeleze amejionea nini hakupokea.

Hata hivyo, hakuna mtu yeyote kutoka LUGUMI ambaye amekuwa tayari kuzungumza ingawa vyanzo vya habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi vimesema kwamba utekelezaji wa kazi ya kufunga kompyuta hizo aina ya Dell umeanza.

“Unajua hili ni agizo na amri ya kamishna mmoja wa makao makuu. Kuna gari lililofuata vifaa hivyo makao makuu na kompyuta hizi zilifika hapa Jumatano na zikafungwa Alhamisi, lakini kama nilivyosema haziwaki na hata askari hawana mafunzo ya kuzitumia,” alisema mpashaji mwingine aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Mtoa taarifa huyo alisema uharaka wa kufunga mashine hizo unafanywa ili kujiandaa kwa ukaguzi wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wanaotarajiwa kupita wilayani na mikoani kuthibitisha uwepo wa mashine hizo. Kwamba watakapofika wakaguzi wadhani kwamba vifaa hivyo vilikuwapo tangu awali wakati si kweli.

‘’Ndugu yangu, huwezi kuamini kompyuta za LUGUMI zimewasili hapa mkoani kwetu (Geita), lakini sasa zimeletwa kwa lengo moja tu kuwahadaa wakaguzi kwamba zilikuwepo tangu awali wakati si kweli. Hizo kompyuta zililetwa Jumatano wiki iliyopita na zilifungwa Alhamisi na mbaya zaidi haziwaki, yaani ni mbovu,” alisema mtu huyo.

Mjumbe mmoja wa PAC aliwahi kulalamika kuwa kuna mchezo unachezwa wa kukwamisha kamati ndogo baada ya Bunge kuchelewa kutoa fedha za kuwezesha kazi ya ukaguzi kuanza kwa lengo la kutoa mwanya wa kufungwa kwa mashine hizo nje ya muda.

Juhudi za kumpata Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hillaly ili atoe ufafanuzi wa kazi hiyo kufanywa sasa tena na polisi wenyewe, hazikuzaa matunda. Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ndogo ya PAC iliyopewa jukumu la kuchunguza sakata la LUGUMI kwa siku 30, alisema mambo yote yatakuwa kwenye ripoti yao. “Kama wanafunga mashine au hawafungi hilo sijui, we subiri tu tumalize kazi tutatoa ripoti,” alisema.

Habari zinasema tayari kamati hiyo iliyogawanywa katika makundi matatu imekamilisha ukaguzi katika Mkoa wa Dodoma.

Kamati ya PAC ndiyo iliyoibua sakata hilo katika vikao vya kamati vya Aprili, ikinukuu ripoti ya CAG ya mwaka 2014/2015 kwamba kampuni hiyo iliyoingia mkataba na Polisi kufunga mashine hizo haikuwa imekamilisha kazi hiyo.

Pamoja na kutokamilisha ufungaji mashine hizo, LUGUMI ilishalipwa Sh34 bilioni sawa na zaidi ya asilimia 90 ya jumla ya malipo ya Sh37 bilioni za mkataba, jambo ambalo wabunge wanaona ni viashiria vya ufisadi katika Jeshi la Polisi.

Katika sakata hilo, pia anatajwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga akitakiwa ajiuzulu kwa madai kuwa ana hisa kwenye kampuni ya Infosys, ambayo ilitoa ushauri wa kitaalamu kwenye mradi huo, ikiwa imeombwa na kampuni ya Kimarekani ya Biometrica ambayo iliipa Dola 75,240 (sawa na zaidi ya S150 milioni).

Hata hivyo, Infosys imenukuliwa ikidai kuwa Kitwanga alishajiondoa kwenye uendeshaji wa kampuni hiyo mwaka 2010 na tangu wakati huo hajakanyaga kwenye ofisi zao.

MONDAY, JULY 2, 2018
Rais Magufuli ataka uchunguzi mkataba wa Lugumi

Kwa ufupi
Amemwagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kufanya uchunguzi wa mradi huo wa Sh37bilioni

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemuagiza waziri mpya wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kufanya uchunguzi wa mradi wa Sh37 billioni wa ujenzi wa vituo 108 vya polisi ulioingiwa kati ya wizara hiyo na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited.

Amesema Serikali ilipewa maagizo na Bunge kuchukua hatua kwa baadhi wa watu waliobainika kufanya makosa katika utekelezaji wa mradi huo lakini anashangaa mpaka sasa haoni hatua zinazoonekana zikichukuliwa.

Kiongozi Mkuu huyo wa ncuhi ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 2, 2018 Ikulu Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua jana, wakiwemo mawaziri watatu na naibu mawaziri wawili.

“Kuna baadhi ya vitu katika mradi huo havijakamilika, vitu vingine wame-exaggerate (wameongeza makadirio) lakini hakuna hatua zilizochukuliwa,” amesema Rais Magufuli.

Amemwagiza pia kuchukua hatua kwa waliohusika na mradi wa kuagiza magari 777 ya polisi aliyodai yaliagizwa kupia mkataba wa ovyo.

Amesema baadhi ya magari hayo yaliagizwa kama mapya lakini tayari yametembea zaidi ya kilomita 4, 000 na yapo ambayo hayajaandikwa hata tarehe ya kutengenezwa.

“Mkataba wenyewe ni wa ajabu, nimempeleke katibu mkuu (Wizara ya Mambo ya Ndani) Meja Jenerali sikufanya makosa, nimefanya kwa makusudi. Ninaposema mkataba ni wa ovyo najua ni wa ovyo. Niliowapeleka pale hawakuyaona haya,” amesema Rais Magufuli.

FRIDAY, APRIL 22, 2016
PAC hands over its report on Lugumi to Speaker Ndugai

National Assembly Speaker, Job Ndugai

In Summary
In 2011, police entered into a contract with Lugumi Enterprises to install 108 fingerprint reading machines at 108 district police stations across the country, but only eight machines have been installed out of which only two are operational

By Athuman Mtulya ; @mtulya ; [email protected]

Dodoma. The Parliamentary Public Accounts Committee (PAC) has handed its preliminary report on investigations into the Sh37 billion forensic contract scandal between Lugumi Enterprises Ltd and the Police Force to the National Assembly Speaker Job Ndugai, The Citizen has been reliably informed.

One member of the PAC confided with this paper yesterday saying after the committee’s Wednesday meetings, they decided to write to Mr Ndugai a summary of their findings and presented to him names of MPs who would form a subcommittee to dig further on the matter.

“The speaker is expected to give his approval, and then the subcommittee will be given all technical, financial and logistical assistance by the National Assembly to conduct further probe on this case,” said The Citizen’s well-placed source, adding: “This issue is very thorny, and it involves some big people in the system and that makes it more complicated, but at the same time interesting.”

Section 117 (18) allows any parliamentary committee to form a subcommittee for a better execution of its responsibilities.

However, when confronted by reporters yesterday, PAC deputy chairman and Sumbawanga Urban MP Aeshi Hilary neither confirmed nor denied about the matter, only saying they were still busy probing the matter and they would come out tomorrow and tell the public how far they had gone with their investigations.

“This is a delicate matter that needs a serious care, and that’s what we are doing at the committee level. I know this matter has gained public interest, but there’s still work to be done and tomorrow (Saturday) I will personally say what is supposed to be said about what we have found so far and the future of our investigations,” he said.

However, according to our source, the committee decided to form a subcommittee to find clear answers after failing to get them on Wednesday from the permanent secretary of the Ministry of Home Affairs Major General Projest Rwegasira.

“The permanent secretary could not give most of the details that we were looking for to connect the dots. The subcommittee will then be dispatched to find all the remaining questions and it will move all around the country to find them, and present them before Parliament for deliberations,” said our source.

In 2011, police entered into a contract with Lugumi Enterprises to install 108 fingerprint reading machine at 108 district police stations across the country, but only eight machines have been installed out of which only two are operational.

Lugumi Enterprises Limited said in a press statement on Wednesday that media reports putting it at the centre of the scam were ‘false’, asking the public to ignore them.

The company also denied that its CEO, Mr Said Lugumi, had fled the country, saying he was still in Tanzania getting on with his day-to-day duties.

Kama ripoti kuhusu uchunguzi wa Lugumi ilikabidhiwa tangu April 2016 kwanini dikteta asubiri miaka miwili baadaye ashinikize uchunguzi mpya!? Ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Wabunge iliishia wapi? Kwanini haikufanyiwa kazi kwa miaka yote hii miwili?

Dikteta kakurupuka kutaka kutuzuga Watanzania akidhani Watanzania wote ni wapumbavu. Tunataka uchunguzi wa 1.5 trillions SASA aache longo longo zake.

Ama anataka kuhalalisha jambo mahali au analenga kupata kick kuwa hana tolerance na ufisadi ili kusahaulisha mijadala ya maana kuhusu yeye kushindwa kuongoza.

Mtu wa ajabu sana huyu Mkuu. Miaka miwili baadaye anashinikiza uchunguzi wa ufisadi wa bilioni 37 wakati huo huo hataki uchunguzi wa 1.5 trillion ufanyike!

Kuna mtu anantafuta huku kwa Lugumi si muda mrefu Seth na Rugemalila watapata mate

[FONT=tahoma]Hili la Lugumi nadhani ni mfupa mgumu tuseme kazi haijafanyika kabsa au ndo media attention tu jiwe mbna hataki kusikia habari za 1.5t? [/FONT]

[FONT=tahoma]Analalamika taratibu za manunuzi kutozingatiwa wakati yeye ndio wa kwanza kukuika hzo taratibu kwa kutoa zabuni za pesa nyingi pasipo kuidhinishwa na bunge jeshi la mtu mmoja matokeo yake ni kila mtendaji kushindwa kutumia weredi kazini na kufanya kazi kwa hofu. Mifumo lazima iwekwe sawa sio kujiona yeye ndio kila kitu na ndio mwamuzi wa mwisho wakati tuna mihimili mingine kila siku itakuwa teuzi mpya kwa mwendo huu.[/FONT]

Ishu ya Lugumi iko complicated, haya mengine ni mazingaombwe tu…

Tuna Rais wa ajabu sana! Labda yeye kwa akili yake ya Phd uchwara anadhani sheria za manunuzi Serikalini hazimuhusu.

Hahaha

Ishu ya lugumi Very trick…
Maana hapo unawatafuta maafande, it is impossible

Si maafande tu Mkuu, Prince Kikwete naye yumo kwenye Lugumi je ataguswa?

MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Lugumi, inayodaiwa kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi.

Ridhiwani ametajwa katika habari hizo kuwa ni mmiliki wa kampuni ya Lugumi pamoja na wamiliki wengine ambao ni Said Lugumi na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema.

Akizungumza na gazeti hili, Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete alisema yeye hahusiki na kampuni yoyote ya Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo.

“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.

Ridhiwani alisisitiza kuwa hana uhusiano wa kibiashara na mtu huyo na kwamba hafahamu ni kwa nini amehusishwa na kampuni ya Lugumi.

“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani.

Alisema jambo hilo bado liko ndani ya Kamati ya Bunge na baadae ameliona kwenye magazeti ya juzi kuwa Jeshi la Polisi litatoa taarifa yao, hivyo asingependa kulizungumzia kwa undani. Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi.

Kamati hiyo ilipokutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema jeshi hilo

mwaka 2011 liliingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima ambavyo viko 108.

Alisema mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote ili hali vituo vilivyofungwa mashine hizo ni 14 tu, kati ya vituo vyote 108.

Ridhiwani alisema angependa jamii ifahamu kuwa hana uhusiano na kampuni hiyo kwa kuwa hafahamu kabisa hata malipo yaliyofanywa kati ya Serikali na kampuni ya Lugumi anasikia tu kama ambavyo watu wengine wamesikia.

Chanzo: Habarileo

Hoja ya Lugumi huko Bungeni ilifungwa very unceremoniously na kwa mabavu wakati ambapo dalili za Bunge tamed zilianza kuwa dhahiri. Wenye mapenzi mema na nchi hii walisonoshwa na jinsi uchafu wa Lugumi ulivyokuwa swept under the carpet kipindi ambapo vita dhidi ya ufisadi inapigiwa chapuo. Kwamba all this time ni Waziri husika ndiye hajachukua hatua is interesting revelation. Methinks, at least kwa kipindi chote hicho hakukuwa na political will ya kufuatilia kashfa ya Lugumi. Na Rais wetu alivyokuwa mtendaji asingenyamaza muda huu wote.

Kampuni ya Lugumi Enterprises ltd inamilikiwa na Said Lugumi
Kapilima ni rafiki yake Charles Kitwanga
Kitwanga ni rafiki yake Said Mwema
Said Lugumi ameoa mtoto wa Said Mwema
Said Mwema ameoa kwenye familia ya JK
Ridwani ni mtoto wa JK
connect dots…

https://www.ippmedia.com/sw/habari/sakata-la-mkataba-lugumi-bunge-mtegoni

Hali tete Sakata la lugumi

lugumi*Vigogo Mambo ya Ndani wahojiwa kwa saa saba

*Wapambe wake wafanya maigizo kwa waandishi Dar

NA WAANDISHI WETU, DODOMA/DAR ES SALAAM

SAKATA la mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, limezidi kuwa tete baada ya vigogo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhojiwa kwa saa saba na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) mjini Dodoma jana, huku mmiliki wake, Said Lugumi akiwapiga chenga waandishi wa habari Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Dodoma jana, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeishi Hilaly, alisema kamati yake iliwahoji vigogo wawili wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kwa sababu wao ndio watendaji wakuu.

Alisema watendaji waliowekwa kitimoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (D/IGP), Abdulrahman Kaniki.

Aeshi alisema licha ya kuwahoji viongozi, suala hilo bado ni zito na kamati yake itatoa maazimio yatakayofikiwa leo saa sita mchana.

“Tumewahoji watendaji hawa wakuu wa wizara, suala hili bado zito tunawaomba muwe na subira kesho (leo), tutawapa taarifa za maazimio yatakayokuwa yamefikiwa na kamati yangu.

“Mpaka sasa kazi ni ngumu mno, tunaendelea kutafuta ukweli wa jambo hili, hawa walikuja na wataalamu wao.

“Kikubwa kila hatua ambayo tunafikia, lazima tumwarifu Spika wa Bunge ambaye ndiye anayetoa uamuzi juu ya jambo lolote linalohusu Bunge. Siwezi kusema lolote leo (jana), naomba mridhike na hili ninalowaambia kwanza,” alisema Aeshi.

Alipoulizwa Aeshi kama Lugumi ameitwa mbele ya kamati yake, hakuweza kuzungumza baada ya ofisa mmoja wa Bunge kumfuata na kuambiwa anaitwa kwa Spika.

KATIBU WA BUNGE

Kutokana na hali hiyo, MTANZANIA ilipomtafuta Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah ambaye suala la Lugumi bado lipo PAC, alisema kamati hiyo, ikimaliza kazi yake itatoa taarifa za maazimio yaliyofikiwa.

KATIBU MKUU AGOMA

Waandishi walipomfuata Meja Jenerali Rwegasira ili kujua alichoitiwa na kuhojiwa na Kamati ya Bunge, aligoma kwa kusema hayuko tayari kuzungumzia suala hilo.

“Siko tayari kuzungumzia suala hili, kwanza nikiongea mnaninukuu vibaya kwa maneno ambayo sijasema,” alisema Meja Jenerali Rwegasira na kuondoka.

MAIGIZO YA LUGUMI

Jijini Dar es Salaam, mfanyabiashara anayemiliki kampuni hiyo, Said Lugumi, ameitisha mkutano wa waandishi wa habari uliogeuka kama maigizo baada ya ‘kupotea’ ghafla na badala yake wakaibuka waliotajwa kuwa wapambe wake.

Waandishi walijitokeza kwa wingi kwenye chumba cha mkutano kuanzia saa 5:00 asubuhi ambapo walitangaziwa kuwa mzungumzaji mkuu atakuwa Lugumi.

Wakati waandishi wakiandelea kumsubiri, mwandaaji wa mkutano huo, Benny Kisaka aliwaambia kuwa Lugumi na watendaji wake wamewasili eneo hilo, lakini kwa kuwa muda bado, wamekwenda ofisini kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept, Juma Pinto kwa ajili ya kusubiri muda ufike.

Katika hali ya kushangaza, Kisaka aliwakabili waandishi na kuwataka waondoke ukumbini, warudi saa 9:00 alasiri kwa sababu Lugumi na wenzake wana mazungumzo.

“Waandishi nawaomba muondoke mrudi saa 9, tena mzingatie muda ili tuwahi kumaliza tuendelee na majukumu mengine ya kazi,” alisema Kisaka.

Ilipofisa saa 9 mchana, alijitokeza Mhariri wa gazeti la Sauti Huru, Albert Kawogo na kuwaambia waandishi kuwa Lugumi amepata dharura, ameelekea mkoani Dodoma ambako ameitwa na viongozi wa Serikali na kuwataka wachukue taarifa iliyoandaliwa na waondoke eneo la mkutano.

Baada ya kusema hivyo, waandishi walimuuliza Kawogo, nani mwenye dhamana ya kujibu maswali ya waandishi yaliyoandaliwa kwa ajili ya Lugumi.

Akijibu, Kawogo alisema: “Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kujibu maswali yanayomhusu Lugumi, nasisitiza mnapaswa kuondoka kwenye ukumbi, hakuna tena mkutano.

“Lugumi hawezi kuja tena kwenye mkutano huu, amepata dharura anakwenda Dodoma, ameitwa huko na viongozi wa Serikali, chukueni ‘press release’ muondoke, hakuna mkutano tena, mimi sina mamlaka ya kumjibia maswali yake, ndiyo maana ametoa press release, mtasoma humo.”

Alipomaliza kusema hayo, aligawa karatasi hizo kwa waandishi wa habari na kuondoka bila ya kutoa maelezo yoyote yanayohusu sakata hilo, hali iliyosababisha kujitokeza minong’ono ya waandishi wakihoji kwanini Lugumi hakutokea kwenye mkutano huo na Kawogo ni nani yake.

TAARIFA ILIYOTOLEWA

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Lugumi, Juma Sabury, ilisema Lugumi hahusiki na tuhuma zinazoelekezwa kwake.

Kampuni hiyo inadaiwa kuingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011 na kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo 108 nchini kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Lakini hadi sasa, kampuni hiyo imefunga mashine hizo katika vituo 14 tu Dar es Salaam na kulipwa Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha zote.

Taarifa hiyo ya Sabury inasema kampuni hiyo imetekeleza mkataba huo kwa kushirikiana na wabia wao.

Alisema kama kuna mgogoro katika utekelezaji wa mkataba huo, jeshi hilo lilipaswa kuwasilisha taarifa ya malalamiko kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ili aweze kuingilia kati.

“Kwa mujibu wa mkataba wetu, hatupaswi kujitokeza hadharani kulalamika, tunatakiwa kuwasilisha malalamiko yetu kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), siyo sisi wala jeshi hilo,” alisema Sabury.

Sabury alikiri mwaka 2011, kampuni hiyo iliingia mkataba na jeshi hilo kwa kufunga mitambo ya utambuzi kwa kutumia alama za vidole katika vituo vya polisi nchi mzima, vikiwamo vya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Mkataba huu tuliutekeleza kwa kushirikiana na wabia wetu katika kuhakikisha mitambo hiyo inafungwa kwenye vituo hivyo,” alisema.

Alisema kumekuwa na tuhuma nyingi zinazotolewa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii zikimhusisha Lugumi kuwa ametoroka nchini na kuwataka wananchi kuzipuuza akidai ni fitina tu.

“Said Lugumi hajawahi kutoroka wala kukamatwa nje ya nchi, yupo anaendelea na majukumu yake kama kawaida, hizo taarifa zinazosambazwa si za kweli, ni huzushi na kwamba zinapaswa kupuuzwa,” alisema.

TAKUKURU NA LUGUMI

Jalada la mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi limetua mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili uchunguzi zaidi.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli, alisema jalada la uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo liko mikononi mwao na wakikamilisha watawasilisha kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa ajili ya hatua zaidi.

Taarifa hii imeandaliwa na Bakari Kimwanga (Dodoma), Patricia Kimelemeta na Grace Shitundu (Dar es Salaam)