He has been given wings and he is flying.
Maafisa wa polisi wamenasa bangi yenye thamani ya shilingi milioni 1.2 katika eneo la Mwabila, Wilaya ya Kinango.
Maafisa hao walisema kuwa bangi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutumia gari dogo aina ya Fielder kuelekea mjini Mombasa.
Polisi hao walisema kuwa walishuku gari hilo kufuatia fununu walizopata awali.
Waliokuwa katika gari hilo walitoroka na kuliwacha walipogundua wanaandamwa na polisi.
Akithibitisha kisa hicho siku ya Jumatano, Naibu kamishna wa kaunti Kenneth Gitonga alisema kuwa uchunguzi umeanzishwa kuwasaka waliokuwa wakisafirisha bangi hiyo.
Gari hilo lilikuwa likisafirisha zaidi ya misokoto elfu sita ya bangi.
[ATTACH=full]29859[/ATTACH]