Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za heri kwa Watanzania wote kuelekea maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanyika tarehe 9 Desemba, akiwaombea amani, umoja na sikukuu njema.
Wakati huohuo, Serikali imeshauri Watanzania ambao hawana ulazima wa kutoka siku hiyo kupumzika majumbani mwao. Ushauri huo umetolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba.