Tarehe 9 mwezi wa Agosti wakenya walienda kupigia viongozi wao kura. Raila Odinga alikuwa mmoja wa wale waliokuwa wanawania kiti cha urais cha nchi hii akiwa na wenzake William Ruto, Waihiga Mwaure na George Wajackoyah. Ruto aliibuka mshindi lakini Raila akukubaliana na matokeo hayo. Aliwasilisha kesi katika mahakama ya upeo ya Kenya.
Mahakama ya Kenya ilieza kusikiza kesi kuhusu uchaguzi na ikaja kwa uamuzi kuwa Ruto alishinda uchaguzi wa urais bila udanganyifu wowote. Tarehe 13 mwezi huu, Ruto ataapishwa kama rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya.
Mimi kama mmoja wa wakenya, nilimpigia kura Raila Odinga na nilikuwa naonelea kuwa ni vizuri Raila aingie uongozini hata kama ni muda wa miaka mitano. Raila amepigania demokrasia ya nchi hii. Ameweza kuleta sheria ambazo zinasaidia nchi nikaona ni vizuri apate nafasi hata ya kuonja kiti cha urais ndipo aeze kustaafu kwa amani lakini maishani hupati kile kitu huwa unachokitaka. Raila hakushinda kiti cha urais na tunafaa kukubali hayo. Niliskia vibaya sana na nikamuonea huruma alipopoteza uchaguzi wa rais.
Kama haikuwezekana naonelea Raila angeenda nyumbani apumzike. Miaka imesonga sana. Ana umri wa miaka 77 mwaka wa 2027 atakuwa na umri wa miaka 82. Ukiwa na umri wa miaka 80+ wewe tayari ushakuwa babu na anafaa aanze kuwalinda wajukuu wake. Raila atawekwa kwa kumbukumbu za Kenya kuwa kupigania uhuru na demokrasia ya nchi hii.
Ni hayo tu kwa sasa.
Leta transleshen in English mdau.
Jifunze Kiswahili ghasia
[ATTACH=full]464381[/ATTACH]
Hakukubaliana
Raila alionea Wakenya huruma alipojaribu kupitisha mswada wa BBI?
Hii ni nakala chafu
:D:D Nipee hongera. Nimejaribu kuongea Kiswahili sanifu
Hongera walah bin @Kuna Vitu Sipendi umekua kama wale wa Jamii forum
Rayila hajapigania Demokrasia, amepigania mamlaka na madaraka .
Ni malizie hio mwizi ya ngombeee.
:meffi::meffi::meffi::meffi:
[ATTACH=full]464470[/ATTACH]