Polisi na Barabara

Baada ya kutokea vifo vya watoto wa UDSM na staff, amejitokeza mkuu wa polisi na kudai ambulance na magari ya serikali yanaongoza kusababisha ajali kwa kupita njia za mabasi. Sasa leo tu nimeona magari ya majaji wawili na gari lao polisi, na msafara sijui wa nani ; wote wametumia njia ya mabasi. Tofauti baina ya kusema na kutenda ndilo tatizo letu kuu la kisheria Tz

Tatizo sheria zinapowekwa zinadhaniwa kulengwa kwa raia wa kawaida. Mfano barabara za kule posta hasa ile ya sokonne drive utakuta Magari yenye plate no. STK, SU,STL,STJ etc zinatumia road in opposite way na hakuna Trafic anayasimamisha Magari hayo

Tuliyowapa madaraka na wakapata mamlaka wanavunja sana sheria, na hawafanywi chochote…

Cc: @Mahondaw

Hata barabara za mikoani, hayo magari ya jeshi na serikali huwa hawana kero ya kupigwa camera kama haya nagari yetu…

Kuna mentality mbaya sana kwa watu wenye nafasi serikalini, wao hujiona ni muhimu kuliko binadamu wengine na pia sheria hazipo kwa ajili yao bali kwa ajili ya kuwanyoosha wananchi wa kawaida

Jamani, mavyotusema dah, tutabadilika, huwa tunawahi kuhudumia wananchi

Wapo Viongozi wanaovunja Katiba, Sheria, Kanuni na Utaratibu lakini wanawataka wengineo wazingatie!