KIPENZI WEMA SEPETU.
Peni yangu kurasani, japo mie ni kurutu,
Mtima mahakamani, wakuhenza mwanakwetu,
Hunitoki kinyuwani, nakuita mara tatu,
Kipenzi wema sepetu, nikubali nikuowe.
Nikubali nikuowe, uwe wangu wa hubani,
Posa zangu nizitowe, nakuzileta nyumbani,
Nigande sinidondowe, niputukite ja jani,
Kipenzi wema sepetu, wangu kufa kuzikana.
Wangu kufa kuzikana, nataka niwe mumeo,
Kwa mengi tunalingana, kasoro swala la cheo,
Mlango sijaubana, ngia nitie komeo,
Mrembo Wema Sepetu, unazo sifa za taa.
Unazo sifa za taa, kikweli umeumbika,
Nakuwaza kila saa, kitwani kila dakika,
Mtoto moto wa kaa, nakuhusudu hakika,
Kipenzi Wema Sepetu, naomba nikubalie
Naomba nikubalie, Kenya nakusubiria,
Wenginewe wafukie, njoo tuwe abiria,
Wema usinikimbie, nauli nakutumia,
Kipenzi wema sepetu, mumeo nakuhitaji.
Mumeo nakuhitaji, nakuhitaji mumeo,
Namtuma washikaji, Iddi Ninga wa Koleo,
Toka Dar uje jiji, uje uwone wakweo,
Kipenzi Wema Sepetu, ndoo tufunge akidi.
Njoo tufunge akidi, tuishi hadi kiyama,
Tukazidishe juhudi, tuitwe baba na mama,
Jina naitwa Uledi, kinda mtunga nudhuma.
Kipenzi wema sepetu, ndiwe ua la waridi.
Uledi Bryan
Kinda mtunga Nudhuma
Nakuru Kenya
Simu namba:+254724845351
Email:[email protected]