[FONT=courier new]Uwepo huku KT hauna tofauti na Mwanaume kukimbiwa au kuachana au kuachwa na Mpenzi / Mke wako ambaye ulimpenda kweli ila kwakuwa tu hakuna namna na Wewe ni Mwanaume unahitaji kutimiza haja yako ya Kirijali na Kibaiolojia basi inakubidi tu ufanye ’ tendo ’ hilo hata na Mwanamke ambaye hujampenda au humpendi.
Ninamlaani sana aliyetusababishia huu ’ usumbufu ’ mkubwa Sisi Watanzania Wanyonge ambao tuliuzoea, tuliupenda na tuliuamini sana Mtandao wetu ’ pendwa ’ wa JamiiForums. Kwa hizi wiki mbili tu sasa kutokuwepo kwa Mtandao wa JamiiForums nchini Tanzania kwa sasa naona nimepoteza ’ maarifa ’ mengi na makubwa sana.
Ni ’ madini ’ ya uhakika ambayo nilikuwa nikiyapata ndani ya JamiiForums ndiyo yalikuwa yakinifanya niwe ’ Kijana ’ ninayeaminika na kukubalika mno na Wanajamii wengi maeneo mbalimbali tena na Watu wa ’ rika ’ zote na kulikuwa na uelekeo ambao nilikuwa nikiuona kabisa Kwangu wa kwa jinsi nilivyokubalika na Wanajamii eneo ninaloishi kulikuwa na uwezekano mkubwa mwaka 2020 nikamvua Mtu ’ Jimbo ’ lake la ’ Ubunge ’ ili nami kuanzia mwaka 2020 jina langu libadilike katika kuitwa Mkuu GENTAMYCINE sasa niwe naitwa Mheshimiwa GENTAMYCINE na kwa ’ Uadilifu ’ wangu, umakini na uchapakazi nina uhakika hata katika ’ Cabinet ’ la 2020 ningekuwa ama Naibu Waziri au hata Waziri kamili katika ’ docket ’ fulani ndani ya Serikali ya Tanzania.
Nitaililia na kuimbuka sana JamiiForums kwani sina raha tena japo tumekaribishwa huku ’ Ukimbizini ’ lakini tusisahau kwamba hata iweje au itokee nini Nyumbani ni Nyumbani tu. Huku ’ Ukimbizini ’ Watu ’ tunadanganyana ’ mara wengine wanaiba ID’s za Watu na wanajifanya ni Wao, wale Watu makini ’ Werevu ’ huku tulipo sasa ni wa kuwatafuta kwa ’ tochi ', ule mvuto wa majibizano ya ’ Hoja ’ kama kule JamiiForums huku haupo yaani mambo ni ’ vululu vululu ’ tupu!
Furaha yangu ya 100% itarejea / itarudi tu pale Mtandao wa JamiiForums utakaporejea na kuendelea kutoa huduma zake kama awali.
Nawasilisha.[/FONT]