Nafurahi kukuona Ndege wetu Jamii Forum ukiendelea kupeperusha mbawa zako katika anga la ugenini, si kwamba ninafurahia sana ila hakuna namna kwasababu ndiyo njia mbadala pekee iliyopo kwa sasa, sina budi kutoa shukrani za pekee kwa mtandao wa majirani zetu Kenya kwa kutupatia hifadhi ya ukimbizi katika wakati huu tunaopitia hapa kwetu.Binafsi nimehangaika sana namna ya kujua ni wapi ntaipata Jf mpaka nilipopata taarifa kuwa imepatiwa hifadhi Kenya talk. Ni ombi langu kwa Mungu kuwa hii hali nayo itapita na tutaurudia uhuru tuliouzoea kama Watanzania. Mungu ibariki Jf, Mungu ibariki na kuilinda Tanzania yangu.
I miss you Jf at homeland, don’t worry Jf I believe one day you will be back at your homeland.