Week ilopita nili safiri kwenda Kijiji flani katika harakati za kutafuta Ugali, Nikakuta Mzee mmoja akiwa hadithia Vijana kuhusu vitu mbalimbali…
Na baada ya muda story zikahamia kwa Kakakuona, namna anavyoonekana, shughuri za kimila zinavyofanyika anapoonekana n.k…
Lililoniacha hoi ni kumsikia Mzee akisema Kakakuona anayo Pembe ndogo ndani yake…nimejaribu kumuuliza maswali sikuridhika na majibu yake, nikaona nije kuuliza hapa jukwaani huenda kukawa na Wazee wa Shamba kwa maana waliokulia Vijijini na wanajua mambo mengi!
Ni kweli Kakakuona ana Pembe ndani yake?