NAOMBA UJUMBE HUU UMFIKIE WAZIRI WANGU WA NISHATI.

Leo tarehe 20/06/2018 na Kesho Tarehe 21/06/2018 Kuna huu mkutano wa Anniversary ya Tano ya Gas Summit ya East Africa. Kwa mshangao mkubwa sana katika main speakers hakuna Mtanzania hata Mmoja

Huu ni ujumbe tosha Kabisa kwamba hatuna wabebezi katika secta ya Mafuta na gesi. Naona wakenya wengi sana, wasudan, wamozambique wamepewa nafasi ya kuhutubia katika mkutano huu.

Hili sio suala dogo la kuliacha lipite tu, Nimebahatika kufanya kazi kama mhasibu katika moja ya haya makampuni ya mafuta na gesi na nimekutana na vichwa vya hatari sana kwenye suala zima la mafuta na gesi,

Tunahitaji Elimu, Sio ya Darasani tu. hawa wataalamu tuwapeleke nchi mbali mbali zilizobobea katika secta hii ya mafuta na gesi and they must give results!!! watanzania wengi wanatabia ya kwenda kula Bata wakipata nafasi kama hizi.

kwa maelezo zaidi kuhusu huu mkutano tembelea link hiyo hapo chini.

http://eaogs.com/

ndugu yangu @Pascal Mayalla ukipata nafasi naomba mchango wako kwenye hili.

Pascal Mayalla na yeye yuko ukimbizini?

Tungemshauri awe na ID mbili, Maana asije akapotea kama wengine waliopotea

Wewe unadhani huyu Jiwe anatoa tens kipaumbele katika masuala ya Gas na Mafuta??

Yeye priority yake ipo kwenye Stiegler Gauge ya Rufiji

SO SAD,hata mwakilishi mmoja
KILA MWAKA NI KUJENGA MABARABARA BADALA KUCHIMBA GAS NA MAFUTA

Tanzania ni nchi ya riwaya ya nchi ya kusadikika,hii nchi haijui nini inafanya,ipo ipo tu,raisi wetu mwisho wake wa kusafiri Rwanda,Serikali ya Tanzania inayoongozwa na bwana asiependa kukosolewa haioni umuhimu wa yeye au mawaziri wake kukutana na mawaziri au viongozi wa nchi nyengine ili kupanga mambo muhimu yenye mstakabili wa kuijenga Tanzania kimaendeleo

Haya Masuala ya Mafuta na Gesi kwetu yalianza zamani kuliko ilivyo kwa Mozambique. lakini kwa Jinsi mambo yanakwenda hawa Mozambique wanaelekea kutupiga Bao, Majuzi nafikiri umeona habari ya Exxon Mobil wanaondoka Tanzania kwenda Mozambique. na kwa habari za uhakika watakua na LNG plant kule.

Ikumbukwe hawa Exxon Mobil pamoja na Statoil na Shell ambao wamenunua BG ndio walikua na Mpango wa Kuweka LNG plant hapa Tanzania lakini Mpaka sasa hatujui nini kinaendelea.

@Pascal Mayalla tafadhali tunakuhitaji hapa.

Mimi nashauri tuangalie Jinsi ya Kumtumia Proffessor Muhongo. This guy is one of the Brightest man in Geophysical matters in Tanzania.

Hapana Jombaa Kujenga bara bara nayo ni chachu ya maendeleo. Suala la Mafuta na gesi ni namna tunavyoliendesh tu ndio issue

Katika awamu ya utawala huu,It does’t matter if a man is bright as Albert Einstein kama yumo katika huu utawala basi akili yake ni useless,Jamaa(Raisi) haambiliki,hashauriki…

TANGU UHURU MPAKA MWISHO WA DUNIA:D:D:D:D:D

Lets not Politisize things men

Tunaongozwa na mshamba asiye taka kuelekezwa.

Sera za uwekezaji za TANZANIA ni mbovu sana,nani atakuja kuwekeza katika nchi ambayo sera zake hazifahamiki…

Mambo kama hayo hatuyawezi…

Tushazoea visemina vidogo vidogo vya kwenda kujanza kwenye ma-guest…

Cc: @Mahondaw

That’s our Tz

Undugulization mwingi kuliko ujuzi bongo. hizo mambo hatuwezi acha tu tuendelee kuwa watazamaji

halafu wakirudi bongo kauli zao utasikia “TUMEAMUA, TULIZUNGUMZIA, TU, TU…” Utafikiri walichangia hoja vile

Gas sio kipaumbele

Nimemwona pale Kakuma refugee camp, tulikunywa naye chai kwenye canteen ya UNHCR, mie nikaondoka nikarudi huku Mboloni refugee camp nilikofikia! Sikutegemea kama Pascal Mayalla naye atakimbilia nchi jirani!