Nani kaelewa agizo hili la waziri mkuu Kassim Majaliwa?

Mkuu kama haya mambo unayafahamu au huwa unayafuatilia hii haikupi shida sana!

Kitu unachotakiwa kujua ni kuwa wahanga wa agizo hili sio wale wanaokuwa safari za kikazi, bali wale ambao wapo maeneo yao ya kazi ambao mara nyingi hutumia magari ya umma kufanya mambo yao binafsi, ikiwemo kwenda kwenye vijiwe vya kahawa.

Kuhusu huyo uliyemsema kuwa yuko mbali kama 90km na ikafika usiku akiwa huko, utaratibu ni kuwa anatakiwa apeleke gari eneo la maegesho ya serikali lililo karibu zaidi na sehemu aliyopo baada ya kutoa taarifa. Kama umbali huo ndo wa karibu basi ana wajibu wa kurudi. Halafu kama eneo hilo halina maegesho ya serikali ni dhahili patakuwa interior sana ambako hata dreva mwenyewe hawezi kulala bora arudi mjini.

Lakini kama tulivyosema utekelezaji wa utaratibu huu sio mwepesi maana wakubwa wengi ndo wanaongoza kuuvunja, hususan pale wanapokuwa kwenye ziara za kikazi mikoa tofauti, utakumbuka taratibu zinawataka kutumia magari ya ofisi kwenda safari, sasa ikifika jioni sio rahisi mtu akaenda kupaki gari akatembea vijiweni kwa miguu, ataenda nalo tu!

Tusubiri kanusho…

Cc: @Mahondaw

Siku ya kutembea uchi ndio unakutana na mkweo.

Ngumu kutekelezeka

Hivi alikuwa anawahutubia akina nani hao wanaopigia vigelegele jambo la kipumbavu kama hilo? Yaani matanzania tumekuwa mapumbavu sana awamu hii!