Nakuja kuoa Kenya,nipokeeni

Si mtanikubalia ?

            NAKUJA KUOA KENYA

1)Acha niseme ukweli,nitue huu mzigo
Naende kuoa mbali,huku nakupa kidogo
Nawabwaga chini chali,nashusha yangu mapigo
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

2)Huku wengi omba omba,wanapenda kutuchuna
Wanapenda omba omba,kwa hilo ninawachana
Japokuwa wapo bomba,ila upendo hakuna.
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

3)Wabongo waringa sana,wataka mahari kubwa
Wanapenda vilivyonona,kuku baga na ubwabwa
Kwa mahari washindana,shindwa wakwone jibwa
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

4)Wanaweza kutajia,mahari mamilioni
Kama wanatukomoa,twajifanya hatuoni
Kenya nakuja kuoa,make nimpe thamani
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

5)Hawana penzi la kweli,huku wanawaza pesa
Jitie we ujahili,uone watakutesa
Nakuja kuoa mbali,bila jicho kupepesa
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

6)Sura zao za dukani,tena ghali waziuza
Najitoa mashakani,sitaki mauza uza
Wajiona wa thamani,na utu waupuuza
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

7)Nimechagu wakenya,wanaojua kulea
Namanga ninaipenya,Nairobi nasogea
Watanga ninawaonya,wamrshaji haribia
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

8)Bongo wanaringa ringa,na midomo wabenua
Nakipuliza kipenga,ili kesho waje kua
Wametupa ya wahenga,yuropa wamechukua
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

SHAIRI-NAKUJA KUOA KENYA
MTUNZI-Idd Ninga,Arusha.
+255624010160
[email protected]

 :meffi::meffi::meffi::meffi::meffi:kinyesi

Niaje Ng’ombe ya Magufuli

Jaribu @Shiroe

utakuwa we ni boy,sa usiwe na wasi wasi,nakuja oa mmoja tu.

Asante,kwani kuna shida ?

Shairi mufti kabisa, Lakini hatukutambui…kula kwenu…

Izo nyang’au utaziweza :slight_smile:

ila nimependa wa Kenya,nataka nipate mrembo mmoja toka kwenu.
Arusha ni karibu sana na Nairobi,hata gharama ya kuja ni ndogo.
nikubalieni please…

Nitazimudu Jo.
si umeona naanza jifunza lafudhi ya Kenya.

La ! Yeye ni dada babkubwa

kivipi ?

Kaza mwendo mkuu nasikia jalio wana kibumbu tamu sana

:eek:

hujajaribu na wewe ?

lahaja.

Nawavuti kasi huku nikijifunza lugha yao muda sio mrefu watakula chambo

Ng’ombe ya magufuli, tuma mshenga

https://www.youtube.com/watch?v=Gr01IsudBNc

hata mmoja si mbaya.

:DHivi wewe ndio ng’ombee:D:D:D @Idd ninga