Mwenendo wa siasa za Magufuli, tulipokosea wananchi, walipokosea viongozi na CCM.

Leo kile kinachoshuhudiwa nchini Tanzania ni sawa na kusema majuto ni mjukuu huja mwishoni. hapa kuna makosa makubwa yalifanywa na maeneo hayo matatu niliyoyataja.

Makosa ya wananchi.
Kule kumpa kura mgombea wa CCM na kuiamini CCM wakati imeshatutenda mara kadhaa hadi kuifikisha nchi kusikojulikana. Kama ni ufisadi ulishapitiliza, kama ni kushindwa mikakati ya kuindeleza nchi ilishashindikana chini ya CCM na kama ni matumaini yalishapotea chini ya CCM, ilikuwa ni lazima CCM ingoke kwanza ili tujipange upya.
Hapa kwa kiasi fulani wananchi tulifanya makosa na hiki kinachoendelea leo ni kazi ya mikono yetu.

Walipokosea CCM na Viongozi wao
Tunajuwa kuwa CCM kama chama sasa hivi kuna watu wengi wanajutia ndani ya mioyo. Viongozi wa CCM walifanya makosa sana ya kuendekeza ubinafsi wao wa kutanguliza maslahi yao na kushindwa kuja na mikakati imara ya kumpata MBADALA WA YULE WASIYEMPENDA(LOWASSA). Makosa haya yaliiweka rehani nchi kuanzia siku ile hadi leo pale kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM chini ya Kikwete ilipofanya maamuzi ya visasi na ikawa hawakujiandaa na mtu ambaye angekuwa muafaka kwa nchi kama Tanzania. Wengine tulishajuwa wazee kama Kingunge kujitokeza hadharani kupinga na kumfananisha Magufuli na Nyapara wa Bararara kuwa ndio kazi ambayo ingemfaa na si urais.

Leo baada ya miaka miwili tu yanatimia. Tunashuhudia anguko la demokrasia na umoja wetu. Tunashuhudiua uvunjifu wa wazi wa sheria zetu na katiba unaofanywa na mamlaka za serikali chini ya Magufuli. Tunashuhudia vitisho na ubabe usiofuata weledi wowote zaidi ya uzwazwa. Zilikuwa wapi mamlaka za kiintelijensia kubaini madhaifu ya huyu mzee ndani ya CCM na ndani ya Dola ?

Walikuwa wapi wazee wa mfumo na wazoefu wa itikadi za kisiasa na kidiplomasia wa Tanzania ?

Hongera Kenya Talk kwa kutufariji.

Kishada.

Hatuna uhakika kuwa hata hizo kura alizotangaza Lubuva ndivyo zilivyopigwa. WALAANIWE WOTE WALIOHUSIKA kuhakikisha Sizonje yupo hapo alipo.

Hmm!..

Wote hao uliowataja ndio wale wenye maslahi na CCM. Kwa hio bado ni CCM au viongozi wa serikali wenye mamlaka ndio nao wanabeba hii dhima.

Mkuu pamoja na majuto ni mjukuu, ilikuwa lazima huyu kichaa aingie madarakani kutupa na kuonyesha shubiri ya kutokuwa makini kwenye kuchagua viongozi. Hii ni kuanzia kwenye kuteua, sheria za uchaguzi, usimamizi wa uchaguzi. Kikubwa zaidi tumeweka rehani elimu yetu ya kawaida ya kudadavua hoja. TUNALO

Nchi ya ajabu sana hiyo!!!

Na waliofanikisha goli la mkono wameanza kukuri wenyewe.Wanajua walichofanya na naamini yamewatokea puani kwan nao wanaisoma #

Umesema vyema mkuu, funzo jingine nikutofanya masihara na mambo muhimu kama ulivyofanywa mchakato wa katiba mpya pamoja na garama zote zilizotumika.Naamini ule mchakato usingevurugwa tungekuwa na taasisi imara na huyu kichaa asingekuwa na nguvu hivi.

Kuichagua CCM ni sawa na kujivisha mabomu.[ATTACH=full]176013[/ATTACH]

Nape alikiri kuwa ni Goli la mkono limemuweka kwahiyo lawama zoote ziende kwa lubuva na Nape

Haraka haraka haina baraka …ni ile kasi ya kutafuta nani anafaa kuongoza wakati tayari maji yako shingoni.Huyu jamaa hakufaa kabisaaa kutuongoza ila ni juhudi za akina Nape na Mkapa kuokoa jahazi kuzama.

Tutakutana 2020. Lazima heshima irudi

Tuache kucheza kamari!!haiwezekani kiongozi mkubwa kama Rais aingie kwa bahati mbaya,mwenyewe alishakiri kuwa alijaribu tu.

Kuepo kwake ni kwa ridhaa ya goli LA mkono sio kura za wananchi

Watanzania sisi tulishalogwa wote, hatuna mtu rasmi WA kukemea,kuonya na kukaripia viongozi WA juu, tangu baba WA taifa hili aondoke duniani Basi kila kitu klikwenda mrama.hata viongozi wastaafu WA serikali na WAKUBWA wamefumbwa vinywa vyao.

Binafsi sikumpa kura, na wengi ninaowafahamu hawakumpa kura ila utawala uliokuwepo kipindi kile ulihakikisha anaingia madarakani "by hooks and crooks" anatawala nchi kimabavu kama alivyoingia madarakani kimabavu. Makosa tunayoendelea kuyafanya ni kumwacha aendelee kufanya anavyotaka, tusipoangalia na tusipomdhibiti sasa huyu mtu ataendelea kuwepo madarakani mpaka kifo kimtenganishe na siasa…dalili ndio hizi zimeshaonekana, bunge liko off, mitandao imezimwa, magazeti na vyombo vingine vya habari haviko huru, uchumi wa unapumulia mashine, maisha hayaeleweki… nini kitakachofuata? Tusipomdhibiti huyu nduli sisi na vizazi vyetu tutaendelea kuumia… wakati wa mabadiliko ni sasa

mkuu
wananchi walijitahidi kwa kweli katika kuto kumpa jiwe kura…si unajua kuwa wamekiri kuwa walitumia jiwe la mkono…kosa kubwa lipo kwa viongozi wa lumumba kumpa taifa mwendawazimu…nadhani paschal mayalla aliwaambia mapema hata kabla ya mkutano mkuu wa lumumba uliompitisha jiwe

Mkuu,Unafikiri nini Watanzania tufanye kuepukana na hili janga 2020?!