Mwendokasi unaongeza kasi ya mateso kwa wakazi wa Dar.

Mwendokasi umekuwa wa mateso kwa kasi kubwa sana.
Jana kulikuwa na wageni toka nchi zilizoendelea walipanda usafiri huu wa mateso. Waliminywa sana hadi walibadilika rangi.

Watu walikuwa wanashuka kupitia madirishani kama usafiri wa Mbagala sababu watu walikuwa wengi kituoni na mabasi hakuna sasa likisimama liliojaa tayari watu waliopo kituoni wanalazimisha kuingia.

Ugonjwa wa ‘network inasumbua’ unaanza kuwa maarufu.

Karibuni gari zitakufa na vioo vitavunjwa ovyo.
Mradi umetelekezwa wakati imewekezwa pesa nyingi watakayoilipia walipa kodi wa Tanzania.

Akija raisi mwingine naye aje kuipotezea miradi mizuri ya awamu hii.
Raisi ajaye apuuzie SGR na bombardier zote?

Na amini Mh. Magufuli anauwezo wa kusimamia mradi wa UDART BRT usife lakini kama tu hataacha yanayo endelea sasa yaendelee miezi 5 ijayo, maana hadi kufikia muda huo uharibifu mkubwa na hasara isiyodhaniwa vitakuwa vimeshatokea.

Mkuu leo nili kaa kituoni zaidi ya Dk 40 kila gri ikija iko full joto kali sana kila abiria akishuka kinyasho kina mtoka

Sijui magari huwa wana yapeleka wapi abiria wengi mabasi hakuna mashine hazi fanyi kazi pale ukitaka ku swap

Vituo havi tangazwi kero kero bora daladala zetu tuna minyana lkn uhakila wa usafiri upo

Poleni sana watanganyika wenzangu

ila huo mradi ambao hauna ushindani utawatesa sana watu wa Dar. Nasikia magari saa mbili usiku yanaenda kulala.

dar es salaam ina uhitaji wa zaidi ya mwendokasi

Poleni sana…

Mimi nilishasema kuwa, ukiachana na sauti ya yule demu anayetaja vituo yale mabasi hayana kitu kingine cha maana

Aiseee!

Kwa mfano?

Magari ya mwendokasi bwana kwa sasa naona yalipata hitilafu hasa kipindi kile cha mvua, lakini naona wameshindwa kuyafanyia maintenance ili mengi yaweze kirudi barabarani na yale ambayo tuliambia yamefika mengi kama 70 pia naona hayajaingia barabarani mpaka leo sasa sijui sababu ni ipi, kwani kwa sasa magari yamekuwa ni machache na vile vile wanashindwa kujipanga vizur(timing) kwani muda wa kutoka maofisini wafanyakazi wengi unaeleweka saa kumi kasoro mpaka saa11:30, sasa unakuta muda huo magari mjini yapo machache ndio husababisha mambo ya kujazana vituoni na hivyo kushindwa kucontrol population. Hivyo basi hata kama magar ni machache basi wajitahidi kujipanga na kuwa na timing nzur.

wako wenyewe tu bila ushindani mradi umewashinda je wakiruhusu daladala kwa njia hizo si ndio utakufa kabisa

Ni

Ni kweli waruhusu na daladala zipite humohumo. Nahic itakua njema sana.

Tz itasonga kama tutafanya Hivyo.

Then back to Kifo kama cha Uda vile.

Sio priority yetu hiyo. Priority yetu ni Kufunga mitandao.