Mwanamke ni Kazi

Kuna tabia jamani ambazo zinaudhi tena zinachukiza. Mwanamke ni kioo cha jamii na hivyo basi unapaswa kuwa mfano bora. Waswahili husema mcheza kwao hutuzwa lakini ukiwa mzembe utapigwa mfano na nani?

Mwanamke aliyeiva hurauka asubui pale nyumbani na kuchacharika. Vijikazi hapa na pale kuhakikisha kila kitu kiko sawa bin shwari. Lakini kuna baadhi ambao wanatabia za kushangaza. Yani akiamka tu, simu mkononi atasakura kwenye mtandao mpaka anajisahau. Haendi kuoga wala kusafisha nyumba. Kila kitu anaitisha akiwa pale pale kitandani utadhani mgonjwa kumbe ni mtu na siha zake.

Jameni! Ukiwa na tabia kama hizo kesho utawezaje kumudu majukumu ya nyumbani kwako? Sio wanawake wote walionatabia kama hizi lakini wapo baadhi ambao bado hawajajua maana ya kuwa mwanamke katika jamii. Badilika uishi!

11 Likes

Kweli yako!

2 Likes

Ngoja feminazi watoke Instagram, utaona cha mtema kuni

5 Likes

Unataka kusema nini ngure?

umengonga ndipo …

1 Like

kiswahili kingi!changamua your wife kwa bedroom nautakua tu ukisikia whistles akipanga mambo ya kwake…

2 Likes

Ukistaajabu ya chawa utayaona ya kunguni…karibu sana @Ngule kwa hiki kitongoji chetu.

3 Likes

Ngule ni nini na ki- NUGU?

Fafanua Mtanzania Magufuli

Is your second name WiFi?.. Because I’m making a Connection!.. Kikikikkkk…

[ATTACH=full]111217[/ATTACH]

2 Likes

Ngule bin Ngule amegonga ndipo.

1 Like

Acha ufisi kafuda.

1 Like

ebu nichangamue wangu saa hii naskia akiitisha sijui maji sijui niletee bag…

Aisee

Muktatha mufti

1 Like

Sisi wenye tunacreate employment kwa kuwa na househelps twaamka nakupata kila kitu on point kwanini tusiscroll mtandao na wifi iko.

1 Like

No comment

:D:D

Sio wanawake wote ni wavivu jameni ndio maana nimetumia neno ’ baadhi’ meaning SOME.

2 Likes