Kwa kawaida baada ya hukumu upande mmoja kwenye shauri huwa una haki ya kukata rufaa kama haukuridhika na hukumu, rufaa hii huwa ina muda maalumu (time frame) kuna siku 14 kuna siku 30 kutegemea na aina ya shauri.
Tatizo lililopo ni kwamba huchukua zaidi ya mwezi kupata nakala ya hukumu kwa utaratibu wa kawaida yaani bila kutumia ushawishi, hii ina maana watu wengi hupoteza haki zao za kukata rufaa na wengine kujikuta wamehukumiwa au wamedhulumiwa, kwani utaratibu wa rufaa lazima uambatanishe na nakala ya hukumu …nadhani hapa mahakama inabidi ijitathmini tena sana, utakuta mtu anapewa siku kumi na nne za kukata rufaa halafu nakala ya hukumu inakuja kutoka baada miezi mitatu justice delayed is justice denied.
Purukushani za mahakama zetu bila mshiko wallahi hutoboi. Kama huna msaada wa mwanasheria anayeielewa mifumo ya behind the scene, lazima uwe na pesa za kutosha.
Haya ndio mambo ya kufanya kama rais jiwe angekuwa na akili sawa sawa za kiuongozi, lakini yeye kutwa anatafuta wapi pa kutafutia kiki za kisiasa
Rais bora na mwenye sifa nzuri za kiuongozi ni yule anayetengeneza mifumo imara ya kiutawala na siyo ambaye kazi yake ni kujijenga yeye pekee yake ili wananchi wamuonee huruma kwa ayafanyayo
Tunahitaji Rais wwenye kuelewa nini maana ya kuwa kiongozi wa nchi, na siyo huyu aliyesukumizwa na wajinga wenzake na yeye bila kufikiri akasukumizika tu
Wenzetu kwa waliostaarabika hujenga mifumo strong na siyo mtu strong kama ambavyo tunaona hawa wezi wa nchi zetu za Afrika wanavyofanya