[SIZE=5]Mahitaji[/SIZE]
[ul]
[li]Ndizi bukoba 2 kubwa zilizokomaa vizuri[/li][li]Karoti 4[/li][li]Butter vijiko 2[/li][li]Kitunguu maji 1[/li][li]Nyama robo[/li][li]Supu ya nyama[/li][li]Maziwa robo lita[/li][li]Cream ya maziwa[/li][li]Mdalasini robo kijiko cha chai[/li][li]Nutmeg robo kijiko cha chai[/li][li]Nyanya 1[/li][/ul]
[SIZE=5]Maelekezo[/SIZE]
[ul]
[li]Bandika nyama jikoni, iive iwe laini na ibaki na supu.[/li][li]Menya ndizi, nyanya, kitunguu na karoti.[/li][li]Chukua sufuria, kata nyanya, ndizi, karoti na kitunguu. Weka vyote kwenye sufuria moja.[/li][li]Weka mdalasini, chumvi, butter na nutmeg kisha weka supu na nyama. Bandika jikoni.[/li][li]Supu ikikaribia kuisha, weka cream, punguza moto acha ichemke kama dakika 5 kisha weka maziwa.[/li][li]Epua, acha ipoe kisa saga. Ipashe kidogo mpe mtoto ale itakayobaki iweke kwenye jokofu.[/li][/ul]