Serikali nzima ilihamia Chato kumzika Monica. Waheshimiwa walipelekwa na Dreamliner kwa gharama ya kodi zetu.
Za kunyapia ni kuwa Monica alifariki siku tatu kabla ya tukio. Imetengenezwa kama tukio la ghafla lililomkuta mtukufu akiwa mapumzikoni kwao. Hii ni katika kufunika yaliyotokea Buyungu yapite na yaliyosemwa na Ubalozi wa Marekani yasahaulike. Lakini Mungu ana mengi, mkurugenzi wa Korogwe akalikoroga.
Si kila aliyekuwa pale alikuwa na uchungu, wengi walikwenda kwa nidhamu ya woga. Bwana yule anajua kuweka vinyongo na ni mtu wa visasi.