Msaada kujilipua nje ya nchi.

habari zenu wakuu, poleni kwa kuwa ukimbizini,
pamoja na kuwa ukimbizini lakini tupeane mbinu za kutoka hapa tulipo jamani, najua kushindwa ni kuacha kupigana sio kubadilisha mbinu. kwa hapa nimepigana na kubadilisha mbinu mpaka basi. sasa kwa wale waliofanikiwa kutoka tanzania na kujishika nchi nyingine please tupeane mbinu na maarifa ya namna ya kutoka hapa Tanzania. pia ni nchi gani ina wepesi walau kidogo wa upatikanaji wa riziki . ??

wakuu tusiwe wachoyo ebu fungukeni popote pale, iwe south, nchi za ulaya, marekani na popote pale. natanguliza shukrani

Mwenzako Emerson Mnangagwa kalipuliwa, tena nchini mwake! Wewe unataka kujolipuwa mwenyewe tena nchi za watu! Amazing.

Jitahidi utafute mazingira mengine hapa hapa Tanzania ambayo unahisi biashara utakayoanzisha itaendana na mazingira hayo…Usikurupukie biashara zinazokuletea definition ya faida kubwa utafeli…Fanya biashara ya kawaida yenye faida ya kawaida itakutoa …Ukishindwa kufanya maajabu kwako usitegemee maajabu yakutokee kwa jirani