Mwanamume mmoja alipokea kichapo kutoka kwa umati uliokuwa umegadhabishwa baada ya kupatikana akila uroda na mwanafunzi ndani ya lori, katika eneo la Mrima, wilayani Likoni.
Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya upili iliyoko eneo hilo pia hakusazwa kwani akina mama walimtia adabu ya kutosha.
Maafisa wa usalama waliokuwa wakipiga doria katika eneo hilo waliwanusuru wawili hao kutoka kwa umati huo, ambao ulikuwa unataka kumuangamiza mwanamume huyo ambaye ni dereva wa lori la kusafirisha mchanga.
“Jamani tunawapeleka watoto wetu shuleni wapate elimu lakini hawa waume wamezidi. Waache wasichana wetu wapate elimu wajisaidia siku za usoni," alisema mkaazi mmoja.
Haya yamejiri siku chache baada ya madai kuzuka kuwa madereva wa lori pamoja na wale wa masafa marefu wamekuwa wakitosheleza ashiki zao kiholela kwenye gari hizo.
Wakazi wa maeneo hayo wameitaka serikali ya kaunti kuweka sheria kali dhidi ya madereva hao, na iwapo wataikaidi, wakabiliwe kisheria.
Wazazi nao wametakiwa kujua mienendo ya watoto wao, kama njia moja ya kuwazuia kuambikizwa na maradhi kama vile ukimwi.
Dereva huyo na ‘mpenzi’ wake walipelekwa katika kituo cha polisi kwa mahojiano…
Team mbisha poleni