Mmiliki wa Jf akubali masharti ya sheria za uendeshaji wa Jf

Sheria ya uendeshaji wa electronic platform inamtaka mmiliki kuwa na real identities za watumiaji wake hata kama kama watatumia anonymous names. Hata hapa Kenya Talk tumejisaji kwa our real email address na our real telephone numbers ambazo zimesajililiwa kwenye mamlaka husika zikionyesha majina yetu halisi na picha zetu halisi. Kenya talk ilibidi i verify kuwa kweli email addresw na telephone numbers hizo ni za kwetu kweli. Hata huko facebook, whatsapp, instagram na mitandao mingine tumejisajili hivyo hivyo kwa our real emails na our real telephone numbers na mitandao hiyo ku verify.

Sasa Jf hawafanyi hivyo. Wao mtu anajiunga tu kwa kutoa age yake na location. Hivyo mtu huyo jf wanakuwa hawa data yeyote ya maana ya utambulisho wake pale inapobidi. Mbona Kenya Talk wanafanya hivyo, kwa nini Jf huko Tanzania inakataa?

Under that circumstance, I don’t think if the slogan of JF could work out, unless they change it! ( Where we dare to speak openly?

Anonymous names zitaendelea kutumika kama ambavyo hapa Kenya Talk zinavyotumika. Jf itatunza our real email address na our real telephone numbers zetu. In the rare event zitakapohitajika kwa amri za mahakama zetu kama sheria yetu inavyoelekeza, Jf wata avail hizo information kwa mamlaka hizo. Hii wala haitaathiri sana slogan ya Jf - itakuwa “where we dare to speak openly but without seriously breaking the laws of our country!” Na hii itarejesha hadhi ya Jf ya kuwa jukwa la Great Thinkers na siyo great waropokaji/ watukanaji kama ambavyo lilikuwa limefika na hivyo kukimbiwa na wengi wa think tanks wa nchi hii. Moderators wa Jf wamekuwa wakipata tabu sana ku moderate contents za jukwaa hili.

Soma kuanzia page ya 11 ndio utaelewa ni namna gani ilivyongumu kutizima matakwa ya hizo kanuni kurupushi@Sungura

Sio kila kitu lazima muteteee bandungu, Kama Taifa tunamikwamo mingi sana, kuongeza mikwamo mingine isiyo kua na afya ni jambo baya sana kwa maendeleo yetu. Mimi naamini hizi kanuni hazijalenga kulisukuma mbele taifa kimaendeleo zaidi ni kuwafurahisha wanasiasa wachache na kwa maslahi yao binafsi. Emu tuwaangalie vijana wa kitanzania na changamoto zao nakutafuta jinsi stahiki ya kuzitatua sio kuongezaa mikwamo isiyo kua na maana.

Kenya siyo sawa na Tanzania tulia hivyo hivyo…

Kenya hata ukimwambia Rais mambo kama salamu atakujibu poa na yanaisha hapo hapo…

Tanzania ukisalimia mambo bila kuanza na mtukufu cha moto utakiona…

Cc: @Mahondaw

Tatizo siyo hilo wala lengo siyo kufanya hayo Bali tatizo ni ukweli kuwa mwiba mchungu,basi.

Mila na desturi zetu haziruhusu kumsalimia baba yako au mtu ye yote mwenye umri kama baba yako kinamna hiyo. Lazima umsalimie “Shikamoo baba”. Na kama wewe jinsia yako ni ya Ke, hiyo shikamoo lazima iambatane na kupiga magoti. Watemi/ watawala wa nchi husalimiwa kwa kupiga magoti (jinsia zote) huku ukisema " Shikamoo wa nyama"!

Hivi unaelewa kesi ya kodi iliyokuwa ikiwasumbua JF huko mahakamani? Sungura unatetea mavi ya nyanya yako, sheria hiyo haifai maana wanataka kufunga watu midomo ili wakipiga hela watu wasiseme!

Acha uongo wewe! Nani amekupa ushahidi wa kwamba watu humu wa kutoka JF wametoa majina yao ya kweli kwa njia moja au nyingine? Huoni aibu kuja kuandika uongo humu?

Na Maxence Melo hawezi kukubali huo ujinga wa watu kumpa majina yao ya kweli kwani anajua fika hilo halitatokea maana hata watu 50 katika members wa zamani hatapata hivyo ni bora servers ziwe nje ya nchi ambapo hii sheria ya kipuuzi na kidikteta ya mitandao haiwezi kuona ndani. Uongo wako peleka Lumumba si humu na pia wewe hujawahi kuwa msemaji wa Maxence Melo au wa JF hivyo ficha ujinga wako.

Nilipoona bandiko ni lako kabla ya kusoma nilitegemea upotoshaji, na kweli baada ya kusoma nimekutana na nilichotarajia. Kwanza hapa Kt ukijisajili wanakuverify kwa email tu na wala sio namba yako. Na kutengeneza email add ni kitu cha dk moja. Hakuna details nyingine yotote ya maana wanayohitaji zaidi ya procedure za kawaida hivyo acha upotoshaji.

Mello hatakubaliana na sheria zenye nia ovu. Usidhani wananchi wote ni wajinga watakubaliana na sheria zenye nia ovu eti kisa zimetungwa na watawala kwa faida ya madaraka yao, na kisha kwebda kupitishwa na bunge lisilojua wajibu wake. Hata serekali ya makaburu ilikuwa ni mamlaka halali na ilitunga sheria za kikatili na wananchi walio wengi hawakuzitii. Unasema eti hili jukwaa likifuata hayo masharti litasababisha watu wenye heshima zao kurejea kwani kitakuwa hakuna matusi. Kama tatizo lingekuwa matusi wala jf isingefungiwa kwani watawala hawajali matusi, bali ukweli unaohatarisha madaraka yao.

Baada ya jf kusitisha huduma zake kutokana sheria yenye nia ovu kuhusu uhuru wa kujiekeza, kuna forums zonapigiwa debe kama tuzungumze forum, bongoforums nk, zimedoda. Mbona hatuwaoni nyie wastaarabu mkienda kuchangia? Sheria chafu zinazotungwa kwa nia ovu hakuna atakayezitii. Sana sana utaona nchi zenye kujua thamani ya wananchi kuwa huru kutoa maoni yao zikitoa platforms zake watu kujieleza kwa uhuru.

Huko nyumbani bakini na forums na media zilizo kimya bila kuhoji iweje bei za mafuta ya kula, sukari, nishati kama mkaa, gas kupanda juu tena kwa sababu ya sera mbovu za serekali. Ajira kupungua na madhila kama hayo, huku bunge na mamlaka nyingine zikiwa hazina uwezo wa kuhoji na kutatua matatizo hayo.

!
!
Acha Kuoposha Wewe. Mimi Nimefungua Email Mpya Nikajiunga Na Kenya Talk. Sijawahi Chochote Cha Ukweli Humu.

!
!
Acha Uongo Wewe Kenge

Nimetumia email fake, hata Id nimebadilisha. Na kama jf yetu haitarudi kama ilivyokuwa mwanzo au bora zaidi kwenye usiri wa information za members, heri isirudi.

Bavicha wanafikra kwamba ni wao pekee ndio waliopo Katika risk kutokana na michango yao; ila hata sisi pia wenye mitazamo kama hii tupo at risk.

Rafiki yangu ambaye ni member Katika mtandao flani maarufu aliwahi kuniambia kuwa alikua anafuatiliwa na vijana wa chama pendwa wakiongozwa na mheshimiwa flani aliyewahi kuwa na tuhuma flani flani; hivyo swala hapa ni kuhakikisha tu watu wanakuwa na matumizi sahihi na yenye tija ya mitandao.

mkuu acha kupotosha ni wapi kt waneverify number yako, Facebook na mitandao mingine option ya number ni kwa ajili ya notification na ku reset password incase umesahau, Hakuna kitu kinaitwa real emails ficha ujinga wako uta juaje hii ni email yangu halisi? ile hali ku create ni within a minute tena hakuna verification yoyote kwa emails kibao

Ni kosa kubwa sana kumuweka rais kwenye nafasi ya baba, ufikiriaji wa namna hii ni wa hovyo. Ndo maana mnawaona wanao hoji mienendo ya rais kama watu walio kosa adabu! kitu ambacho si kweli. Ifike mahali tumwone raisi aliye tumia rasilimali zetu nje ya utaratibu sawa sawa na mkuu wa idara aliiye fuja rasilimali.

ulichokiongea hukijui

Mkuu uko sahihi … Jf italazimika fuata takwa hilo.

We bila shaka ni agent wa jiwe umetumwa huku kuturubuni… tumewakataa tumekuja uhamishoni bado mnatufata fata…shubamit!!!