Mkuu wa upelelezi akana kumhoji Rais Magufuli

[SIZE=5][FONT=times new roman]Thursday, July 12, 2018[/FONT][/SIZE]
[FONT=times new roman][SIZE=5]
Mkuu wa upelelezi akana kumhoji Rais Magufuli

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/4658840/highRes/2041779/-/maxw/600/-/hfmou0/-/upelelezi+pic.jpg
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (kushoto) akielekea kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana kusikiliza kesi inayomkabili ya kutoa lugha chafu. Picha na Omar Fungo
Kwa ufupi[/SIZE][/FONT]
[ul]
[li][FONT=times new roman][SIZE=5]Maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mdee Julai 3, 2017 makao makuu ya Chadema yaliyopo Mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni ni “Anaongea hovyohovyo, anatakiwa afungwe breki.”[/SIZE][/FONT][/li][/ul]
[FONT=times new roman][SIZE=5]By Tausi Ally, Mwananchi [email protected]
Kesi imeahirishwa hadi Agosti 7 na 8 mwaka huu

Dar es Salaam. Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Ilala (RCO), Davis Msangi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hajawahi kumhoji Rais John Magufuli anavyojihisi kutokana na maneno yanayodaiwa kutamkwa na Halima Mdee.
Maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mdee Julai 3, 2017 makao makuu ya Chadema yaliyopo Mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni ni “Anaongea hovyohovyo, anatakiwa afungwe breki.”
Inadaiwa mahakamani kuwa maneno hayo yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Shahidi huyo alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alipokuwa akihojiwa na wakili wa utetezi, Peter Kibatala kuhusu ushahidi alioutoa mahakamani Juni 29.
Sehemu ya mahojiano kati ya wakili Kibatala na shahidi huyo yalikuwa kama ifuatavyo:
Kibatala: Unamfahamu huyo John Magufuli na anaishi wapi?
Shahidi: Anaishi Ikulu.
Kibatala: Uliwahi kwenda kumhoji jinsi anavyojisikia kuhusu haya maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mdee kwa sababu yeye ndiye mhanga (mhusika)?
Shahidi: Sijawahi.
Kibatala: Uliwahi kuwasiliana na mtu yeyote wa Jeshi la Polisi ili afuate utaratibu kwenda kumhoji?
Shahidi: Hapana.
Kibatala: Unafahamu msimamo wa Bunge kuhusu kauli ya Mheshimiwa Magufuli ya watoto wa kike waliopata mimba wasirudishwe shule?
Shahidi: Sifahamu.
Kibatala: Tuchukulie mshtakiwa alitamka hayo maneno, unafahamu iwapo alikuwa akirejea kilichosemwa bungeni au la?
Shahidi: Sifahamu.
Kibatala: Unafahamu chochote kuhusu haki na wajibu wa wabunge?
Shahidi: Sifahamu.
Kibatala: Unafahamu mshtakiwa ni mbunge?
Shahidi: Nafahamu.
Kibatala: Uliwasiliana na Bunge kama sehemu ya shughuli zako za kiuchunguzi?
Shahidi: Niliwasiliana na Spika kumtaarifu kuhusu kukamatwa kwa Mdee kwa njia ya barua.
Kibatala: Umeitoa mahakamani?
Shahidi: Sijaitoa.
Kibatala: Mdee alikaa kwa muda gani chini ya ulinzi?
Shahidi: Siyo zaidi ya saa 48.
Kibatala: Mshtakiwa anatakiwa apelekwe mahakamani muda gani kwa mujibu wa sheria?
Shahidi: Upelelezi ukikamilika.
Kibatala: Unafahamu Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema nini kuhusu elimu?
Shahidi: Kila mtu ana haki ya kupata elimu kadiri awezavyo.
Kibatala: Kuna mahali inasema mtu akipata ujauzito asirudi shule?
Shahidi: Sifahamu.
Kibatala: Unafahamu Tanzania imetia saini mikataba mbalimbali kuhusu mtoto wa shule kupata elimu?
Shahidi: Sifahamu.
Baada ya mahojiano hayo, Hakimu Simba alisema kesi hiyo imetimiza mwaka mmoja na ilitakiwa hukumu iwe imeshatolewa, hivyo aliuhimiza upande wa mashtaka kupeleka mashahidi.[/SIZE][/FONT]
[SIZE=5][FONT=times new roman]Upande wa mashtaka uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 7 na 8 mashahidi wa upande wa mashtaka watakapoendelea kutoa ushahidi.[/FONT][/SIZE]

Unaweza ukawa na charge sheet tuone mashitaka yakoje?

Jamaa kaonyeshwa jinsi alivyo mpumbavu tena hadharani. Sina charge sheet Mkuu hakuna kosa hapa bali ni dikteta tu anataka kudhalilisha watu.

vituko vitupu. kila kitu hajui sasa unatafuta nini huku mahakamani. Unatoa ushahidi kwa kosa lipi? Kosa dhidi ya nani ?

BAK1 soma ka kipande aka uone kuwa hawa watu ni wapuuzi, kutaka kuwasumbua watu tu. Mungu anawaona… ndiyo maana nilitaka kuona charge sheet

In Anthony Willie v Roger Taro (Unrep. N526(M); 19 & 20 November 1985) Amet J, sitting alone, held:

'Mere use and proof of use of threatening, abusive, insulting words, behaviour or gestures is not sufficient, it must be objectively by proper evidence proven that one intended to provoke a breach of peace or whereby a breach of peace was likely to take place. This evidence has to be objective, that is, to others looking on, that the person speaking those words or making gestures or behaviour firstly had the immediate capacity to be able to do an overt act to effect his intention or such as was likely to lead to a breach of the peace; that he was shaping up and moving toward the person at the receiving end with clenched fists or stick or raised hands or picking up sticks or stones – any such overt action to manifest intentions or by which it can be inferred that a breach was likely to take place. Where clearly words are just uttered in the heat of argument with nothing more and shortly thereafter the person using the words walks away – again subjective apprehension is not necessarily sufficient – then clearly no breach was ever likely to take place.’ (emphasis added)

Hao watu wanatumika tuu kama vikokoneo.

Sheet hole government

Siyo ‘Sheet’ … Ni ‘Shit’ …

Hivyo hivyo

Wakili kamgalagaza shahidi
Nalog off

Mashahidi wengi wa Jamhuri wanadhalilika sana

Shukrani sana Mkuu. Watu wamekuwa wapuuzi sana kukubali kutumika na huyu dikteta mswaga ng’ombe na genge lake la wahuni ku terrorize Watanzania kila kukicha kwa kuwabambikia kesi FAKE, kuwateka na hata kuwaua.

Njaa mbaya sana Mkuu mpaka wamefikia kiwango cha kuua Watanzania wenzao ili wapate shibe yao.

Na inawezekana hata ndani ya familia wanachekwa

haya makesi kila siku yanakera sana! kucheza na kodi yangu tu.

Hivi huyu Halima ana Mume…???

Unataka kujaribu kutupa ndoano

Vikokoneo ndo nini mkuu

Aaaaah hapana…Hata kama ni Uchu lakini siyo kwa halima, kwangu bado ni kabinti kadogo…!!!

Halima binti mdogo? basi wewe mhenga mzee

Kweli kabisa hujakosea…Hata wewe ikitokea ukafahamu umri wangu na kuniona utasema nafuata nini humu kwenye Social media…tumekuwa Addicted na hii mitandao tu…!!!