Mkenya acheza kwenye kombe la dunia

Mchezaji Martin Olsson wa Sweden alizaliwa 17 Mei 1988 mjini Gavle, Sweden.

Babake ni raia wa Sweden lakini mamake Maggie Olsson alikuwa Mkenya ingawa kwa sasa ni marehemu. Alitokea Nanyuki, karibu na Mlima Kenya.

Familia yao ni ya wachezaji kwani ndugu yake ambaye ni pacha Marcus Jonas Munuhe Olsson ni mchezaji kandanda na sawa na Martin yeye pia ni mkabaji wa upande wa kushoto uwanjani ambaye pia hucheza safu ya kati.

Dada yao Jessica Olsson, ambaye ni mkubwa wao, ameolewa na mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka Ujerumani Dirk Nowitzki ambaye huichezea Dallas Mavericks katika NBA.
[ATTACH=full]180169[/ATTACH][ATTACH=full]180171[/ATTACH]

Good News

Katuwakilisha vyema Waafrika

Are they “these people”?

Mamake Olsson anaweza ipata

lini mteezeedi atacheza world kepu, tuko na origi na huyu.

You must be better than that…

:D:D:D:D:D

:D:D:D

hahaha nimeosoma hio na accent ya Tz
samahani waiter ongeza grass
mhudumu ongeza grass

Yussuf Yurary Poulsen amekuwa mchezaji wa kwanza wa asili ya Tanzania kucheza katika fainali za Kombe la Dunia, na pia kufunga katika michuano hiyo.

Poulsen pia alitunukiwa tuzo ya Fifa ya mchezaji bora wa mechi hiyo ya Denmark na Peru.

Denmark wamepangwa Kundi C na Ufaransa, Australia na Peru.

Poulsen alifunga bao dakika ya 59, lakini pia alioneshwa kadi ya manjano baadaye.

Denmark walishinda 1-0 Mechi hiyo. Ufaransa walikuwa wamewashinda Australia 2-1 awali.

Poulsen amekuwa akicheza soka ya kulipwa katika klabu ya RB Leipzig inayocheza ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Babake mzazi alitokea Tanga na alifariki kutokana na kansa mchezaji huyo alipokuwa na umri wa miaka sita.

Babake alikuwa akifanya kazi katika meli ya makontena iliyokuwa inatoka nchi za Afrika kwenda Denmark. Ni katika moja ya safari hizo ambapo alikutana na mamake mchezaji huyo, Lene.

Poulsen alizaliwa mwaka 1994 Copenhagen Denmark na uliopita 2017/2018 alicheza katika michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo alicheza mechi nne na kusaidia ufungaji wa bao moja.

Source; Yussuf Yurary Poulsen: Mchezaji wa asili ya Tanzania acheza na kufunga bao Kombe la Dunia 2018 Denmark dhidi ya Peru - BBC News Swahili

umemnyamazisha kabisa huyu mkei