Mfanya biashara App ya Smart Business ni kwa ajili yako

Wafanya biashara wenzangu, nawakaribisha kuweza kusimamia taarifa za biashara zenu kwa kutumia program ya Smart Business. Ambayo itakuwezesha kufanya yafuatayo

  1. Kusimamia taarifa za mauzo - Utaweza kurecord taarifa za mauzo za kila siku, na kuona kiwango cha faida kwa kila bidhaa bidhaa pamoja na level ya kutoka kwake, hivyo utaweza kutambua bidhaa ambazo zinatoka haraka na zenye faida kubwa

  2. Kusimamia taarifa za mauzo ya mkopo, ni rahisi zaidi kuweza kutambua mteja ambaye anadaiwa au aliyeanza kulipa deni lake taratibu na mteja ambaye deni lake limepita muda wa mwisho wa malipo

  3. Kusimamia taarifa za matumizi - utaweza kuhifadhi taarifa za matumizi ya kila siku kwenye biashara, kutambua kundi la matumizi ambalo liko juu zaidi na hivyo itakusaidia kuweka mipango ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kukuza faida

  4. Kusimamia stock/bidhaa zilizopo dukani - Utaweza ku_seti kiwango cha chini cha bidhaa ambacho kikifikia mfumo utaweka alama ya tahadhari kukujulisha kwamba bidhaa hiyo imefikia kiwango ambacho unatakiwa kununua mzigo mwingine, hiyo itakusaidia kuhakikisha kwamba unaleta bidhaa mpya dukani kwa wakati kabla zilizopo hazijaisha kabisa.

  5. Kupata taarifa ya mwezi - Utaweza kupata taarifa ya maendeleo ya biashra yako kwa mwezi husika, ikionyesha kiasi cha mauzo, gharama za bidhaa, matumizi, faida ghafi (gross profit), na faida halisi (net profit)

Karibuni kuweza kutumia mfumo huu ambao kwa sasa unapatikana Google Play store https://bit.ly/smartBusinessApp

Watumiaji wa iOS mfumo utakuwa tayari katikati ya mwezi December, Pia kuanzia January next year mfumo utapatikana pia kwa PC