Meneja nssf temeke atiwa mbaroni kwa rushwa

Ni siku 13 zimepita tangu meneja wa nssf temeke kupokea rushwa na kutiwa mbaroni na pccb.meneja huyo alimuomba rushwa mwanachama aliyekuwa anadai mafao yake na kuzungushwa kwa mda mrefu ndipo alipoombwa rushwa ili alipwe na alipokubali alilipwa mafao yake fasta.meneja alimfuata hadi benki kuchukua rushwa ndipo akapewa hela za moto na kutiwa mbaroni.alifikishwa mahakamani mnamo tarehe 18/6/18 na kuachiwa kwa dhamana.vyombo vya habari havikuripoti taarifa hyo.ajabu ni kuwa bado yupo ofisini.tz ya hapa kazi tu

Uyo meneja anyongwe kabisa

Huyu meneja anaitwa nani vile?

Wanatesa sana wastaafu hawa,ila kwa awamu hii hawezi kuchomoa…

Hawawezi kuchomoa vipi wakati unaambiwa yupo ofisini pamoja na kupokea rushwa

Yuko uraiani atanyongwa vipi?

Ukienda ofisi yoyote nssf watakupa jina lake

Yani kuchukua hela yangu mpaka nihonge tena!!! Huyo panya asingepewa dhamana.

Kwa Tz yetu hii sishangai uyo meneja kuwa uraiani

Ni taratibu tu za kisheria hapo ndio zimemuweka nje na ndio hizo hizo zitampeleka jela,natumai unajujua sheria kidogo…

Loooh dunia hii jamani, yaani mtu hela yake mpaka atoe rushwa jamani? Kuna mwingine alitakaga kuniletea ujinga pale nssf Arusha nikamwakia ile mbaya. Kumbe bahati mbaya zaidi ni mtu wa nyumbani kwetu yaani tunatoka wilaya moja na Kata jirani. Nilipowaka si ndio akajirudi tukaanza kuongea ndipo akanitajia mpaka kijiji anachotoka!! Tukaombana msamaha yakaisha na akanishughulikia fasta vinginevyo nilikuwa naombwa rushwa mimi!! Maana kila nikienda mara oooh, meneja hayupo njoo Jumatatu ukienda tena sijui nini na nini jaribu wiki ijayo hatimaye uvumilivu ukanitoka!!

huyo atakuwb katok kule anakotoka kiparangoto, angekuw ni wa kask lzm angekuw anasota lupango.

Inasikitisha sana…

Palipo na Rushwa hakuna haki… hayo mambo yapo karibia taasisi zote zinazojihusisha na fedha au malipo…

Cc: @Mahondaw

Sasa unataka kila anayesoma habari hii aende ofisi yoyote ya NSSF kuuluzia j8na lake? Wewe uliyekwisha kwenda huki kwenye ofisi yoyote ya NSSF kwa nini usitipatie hilo jina?

Na huyu naye, wapi rushwa inafuatwa?? Huyu atakuwa mzoefu wala haogopi.

lazma anatokea kanda ya nyonyo

Kumbuka karibu kila nafasi kubwa kubwa hapa Tz kwa sasa zimeshikiliwa na watu wasiojulikana. Yawezekana kabisa na Hugo manager ni walewale

Kinachotatiza ni kwa nini hajasimamishwa kazi na mwajiri wake hadi kesi ya jinai iishe? Inakuwaje mwajiri wake hajui kuwa mwajiriwa anakabiliwa na kesi ya jinai wakati wote wako Dar?

Kaka

Na wewe umeijuaje? Inamaana na pccb wamekula rushwa

Tunahitaji uongozi makini ambao utamaliza hili tatizo la rushwa. Serikali ambayo haiendeshi shughuli zake katika uwazi haiwezi kuondoa rushwa.