Ndugu Wana JF ama watumiaji wa mtandao huu, Amani NA Huruma ya Muumba kwenu.
Mara nyingi Tunajiuliza lini JF yetu itarusi TZ hewani, kabla hatujailalamikia serekali kuja NA sheria kali ama malipo makubwa, jee tumejiuliza jee sisi tunaisaidiaje JF.
Wengi wetu ni wanachama wa kudandia NA sio wa kulipa, kuendesha mtandao kama huu unahitaji mtaji, kama tuna nia nzuri hebu Tufanye mchango wa kila mmoja wetu atoe $5/- Kama mchango wa JF kulipia License NA hiyo kodi. wengine wenu mtaleta ubishi eti principals hairuhusu, katika yale matakwa ya TCRA matatu kubali mawil kataa moja.Nishauri like la usajili wa kutumia vibali ukatiliwe.
Wanao niunga mkono kwa huu mchango tujiandikishe majina NA tuuombe uongozi wa JF wafungue number ya Tigo pesa NA account kwa wale waishio njee ya nchi
Mara nyingi tumesemwa kuwa Watanzania ni watu wa maneno mengi NA uwezo ndogo sana, hebu tujitutumue NA tuwaunge mkono JF.
Mimi mwanachama wa CCM wa kulipia NA sio Mshabiki, lakini napenda haki na Najua JF sio chama cha siasa ni a free platform
Jf inahitaji Id yako tu ili wao wapate pesa kutoka sehemu nyingine za wafanyabiashara na sidhani kama wameshindwa kulipa hiyo pesa
Tatizo ni sheria zilizowekwa kwao ndizo si rafiki kwao na kwetu pia
Naona mmeona tumehamia huku sasa mnatumia lugha nzuri ili muwapte mnaowahitaji
ndugu hujamsikiliza melo, shida sio ada bali ni utekelezaji wa hizo kanuni wakijisajili. kwa kifupi hautaruhusiwa kutumia jina fake na ukileta habari yoyote lazima utaje chanzo cha habari yako, yaani kama ni document inavuja toka ofisi ya rais basi umtaje aliyekupa jambo ambalo ni wazi kuwa haliwezekani na ndio maana wanachelea kujisajili
You are Tanzanian Sir, mnapotakiwa kufanya jambo la kheri NA linahusiana NA kujitolea kwa namna moja ama ingine, mnakuja NA vijisababu. NA kwani una tatizo gani hata ujifiche, bora hatuvunji sheria tunao uhuru wa kuwachangia Ndugu zetu
Ukiniambia kosa walilofanya Ben Saanane, Tundu Lissu na wengine wote nitakujibu swali lako. Uhuru huo wa kuchangia mmebaki nao nyie ccm ila wengine tuliobaki (na tunaotaka haki) tumeny’ang’anywa. Mbona kuna watu walikamatwa kwa kuwa tu walitaka kumuombea Tundu Lissu? Sheria gani inakataza kumuombea mtu? Nitajie tafadhali.
Kwa jinsi nilivyokuwa naelimika na JF, hata ningeambiwa niwalipie hiyo ada mwenyewe ningelipia, tatizo wanataka Mshana Jr akileta mada zake za ulozi na wafu aseme chanzo cha habari zake…sasa huko si kutaka kijana wa watu kutoa siri za familia.
Ndugu ushabiki wangu wa kisiasa na wa kisayansi, kwa sababu mie ni mwanachama wa ccm, haimaanishi nikubaliane na kila kitu kinachtendwa NA Serekali, kuna mengi sikubaliani nayo. Swala la Ben Saanane limeniuna sana na ni la kusikitisha Jibu lake lazima lipatikane. Tanzania ni yetu wote, NA siasa sio uadui, we have to Be truthful panapostahili, NA pia siungi mkono kupinga NA kutusi kila kitu kizuri kinachofanywa NA Serekali, there has to balance with what one stands for.
Unaongea nini dogo? Unhamasisha watu kujulikana eti kwa kuogopa kujificha wakati huohuo ww mwenyewe uko huku ugenini na fake ID!! Tunaomba shule zifunguliwe watoto wa viongozi mrudi mnatuchefua.
Muambie huyo kula kulala. Anadhani hapa anajadiliana na wabunge wa ccm ambao waliletewa sheria y mitandao bila kuisoma wakaipitisha kwa maelezo na ufafanuzi waliopewa na Tiss kwenye party caucas. Sasa sheria imeanza kufanya kazi aliyekuwa waziri wa habari Nnape kwenye upitashaji anashaangaa jf iko matatani!
Zamani mwishoni mwa miaka ya 2009 huko tulikuwa tunachangia kuongeza vifaa vya ofisi kama kuweka vifaa maalum vya kupoozea server(cooling system) tukawa tunalipa moja kwa moja kwa max…hata pretor anakumbuka.