Mashairi ya Wimbo mpya wa Joseph Mbilinyi aka Sugu - Mfungwa wa kisiasa #219

Mashairi ya Wimbo mpya wa Joseph Mbilinyi aka Sugu - Mfungwa wa kisiasa #219 (kwa hisani ya Frank J Msaki)


Verse I

Muziki sikuuchagua,bali ulinichagua,nikafanya kweli na Dunia ikanijua,nilichofanya kwa hili gemu mnakijua.
Na Siasa sikuichagua,amini usiamini siasa ndio ilinichagua,na iliponichagua Mbeya wakanichagua,kwa mara nyingine tena Dunia ikanitambua,na wale wasioamini wakaamini imeshakuwa
Na nakuwa imara kama kitu hakijaniua,mfungwa wa kisiasa 219,kuwa Mbunge Mbeya mjini ndio kitu kinanitesa,kwenye hizi verse naeleza kisa na mkasa,mtaji wangu ni watu na sio pesa,hakimu ananifunga na anajua sina kosa lolote nililotenda kisa ni hizi tu siasa.

Political prison Amen!

Chorus

Mfungwa wa kisiasa 219 (aaah)

Mbeya ndio inanitesa (wanaitaka Mbeya)

Najua Mbeya ndio inanitesa

Lakini bado napenda Mbeya inavyonitesa

× 2

Verse II

Wanasema nazungumza mambo yasiyonihusu,wanasema Sugu wataku-shoot kama Lissu,maswala ya Taifa langu kivipi hayanihusu
Hata nikae kimya haina maana ndio nitapona
Kwani ni nini alichoongea Akwilina,risasi ikampitia na leo kesi hakuna.
Wanasema tuna Amani na hatuna,hata uhuru wa kuongea hatuna tena,wananitishia maisha ya kunipeleka jela tena.
Sitaweza kusahau maisha yale, na siwezi kuwasahau masela wale, bila masela wale tusingesonga kwenye kuta za gereza,mimi na mwanangu Masonga tukasonga kwa mwendo wa farasi au kinyonga,siku nazo zikasonga kulala ni kwa miluzi inapigwa kama kipyenga,amani kwa wajela wote na mliosingiziwa kutoka Mungu ndio anapanga.

Chorus

Mfungwa wa kisiasa 219 (aaah)

Mbeya ndio inanitesa (wanaitaka Mbeya)

Najua Mbeya ndio inanitesa

Lakini bado napenda Mbeya inavyonitesa

× 2

Verse III

Mara oooh tunamfunga amemtukana Rais,mara oooh hajamtukana ila tu kamfedhehesha Rais,mara oooh tumemuachia kwa msamaha wa Rais,
Lipi ni lipi semeni moja basi, mara huyu naye kapost kumfurahisha Rais,niko jela CHAKUBANGA akajua Mbeya Rais,mara paap akajua kwanini wananiita Rais.
Na sasa Dunia nzima wanajua mi ni mfungwa wa kisiasa, na kifuani nina namba 219,wanamfunga Mbunge bila kosa alilokosa na matokeo yake wao ndio usingizi wanakosa,kukamata wanasiasa ni ukosefu wa ubunifu,fikra hafifu mawazo siyo yakinifu wanajengea watu hofu wanapotafuta bifu mpaka na maaskofu.

Amen!

Chorus

Mfungwa wa kisiasa 219 (aaah)

Mbeya ndio inanitesa (wanaitaka Mbeya)

Najua Mbeya ndio inanitesa

Lakini bado napenda Mbeya inavyonitesa

× 2

Its another one!

Lakini bado napenda Mbeya inavyonitesa!

Song #219
Artist Jongwe a.k.a Sugu
©Deiwaka Entertainment

Article by Mkoloni

Imetoka lini hii ngoma?

Huu wimbo BASATA wataupiga ban nawaambia.

mistari kuntu viva sugu.ila kale kabarabara ketu ilemi darajani hd lyoto sec umekaano?

Ngoja tuone BASATA wataleta ngonjera gani

Ile kumtaja aliyejipa cheo cha kuongoza Malaika ni BAN tosha. Yaani itapigwa marufuku hata kuusikiliza kwenye simu au youtube

Dah huyu jamaa namuelewa uchanaj style za kina 2 pac hata hizo beat anazotumia namuelewa kichizi harakat sana kwenye mashairi yake… sijutii kumpigia kura

Ebu leta na Audio Kabisa kabla BASATA hawajauJF.

Sugu Moto Chini.

Rais wa Mbeya…hiyo mistari ni tatizo.!

Mashairi ya Sugu yapo kihalisia sana.

Mwenye ka 'audio akatupie humu basi

Isikilize ngoma yenyewe hapa chini[ATTACH=full]176841[/ATTACH]

Kako hapo nimeshakaweka

Asante sana Chief

Huu mziki haudumu

Mistari inaeleweka vyema heko sugu

Oh okay poa