MAPUTO — Serikali ya Tanzania imekabidhi msaada wa tani 500 za mahindi kwa Msumbiji - wakenya wanaumia sana

MAPUTO — Serikali ya Tanzania imekabidhi msaada wa tani 500 za mahindi kwa Msumbiji kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Msaada huo ulikabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, na kupokelewa Maputo na Waziri wa Mipango na Maendeleo wa Msumbiji, Salim Cripton Valá.

Akikabidhi msaada huo, Kombo alisema hatua hiyo inaakisi uhusiano wa kihistoria na kindugu kati ya mataifa hayo mawili uliowekwa na waasisi Julius Nyerere na Edward Mondlane.

Alisema Rais Samia ametuma salamu za pole kwa Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo, na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kutoa msaada inapohitajika.

Katika ziara hiyo, Kombo pia alikutana na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Maria Belvinda Levy, kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Serikali ya Msumbiji ilitoa shukrani kwa msaada huo, ikisema unaonesha mshikamano na urafiki wa karibu uliopo kati ya mataifa hayo.

Tunakaa kuumia mbwa hii ? We have enough rains. Bye motherfucker

Mtu aban hii matako.