Maneno ya dikteta hayo!

Dondoo kutoka alichokisema rais leo

  1. Mradi wa Lugumi kwenye vituo 108 vya polisi.

  2. Magari 777 ya polisi yaliagizwa kupitia mkataba wa hovyo.

3.Mambo ya unifom hewa.

  1. Working permit zinatolewa kama njugu. Mtu hawezi kupata working permit kama hajapita vibali kupitia uhamiaji.

5.NGO’s ziko za hovyo zinafanya mambo ya hovyo. Kachambue. Tunahitaji NGO zinazofanya kwa maslahi ya Watanzania.

6.Kaanze na RPC na RTO wa Mbeya.

  1. PCCB nao wameguswa kidogo kwa kucheza cheza na ufisadi wa NIDA

  2. Nimechoka kutuma rambirambi kabla hata sijamaliza inatokea ajali nyingine. Waziri wa Mambo ya Ndani hatumi hata salamu za rambirambi. Unamsikia yuko kuleeee.

  3. Wafungwa wafanye kazi ya kuzalisha. Hapa Tanzania serikali inapata hasara ya fedha zake kulisha wafungwa. Wafanye kazi iwe ni usiku au mchana, wakafanye kazi.

  4. Mbunge wa CCM unasema bungeni tukienda hivi tutashindwa, si uondoke?

11.Bei ya kahawa Tanzania iko chini kiliko bei ya Uganda. Kama yuko mtu binafsi Uganda anatoa bei nzuri mleteni. Msilazimishe vyama vya ushirika vinunue kahawa.

  1. `Wabunge wote wa CCM ambao hawakuwepo wakati wa kupitisha bajeti watandikwe barua.

  2. Mtwara na Lindi wako wabunge wa CCM 15 niko tayari waondoke bado tutapata quoram ya kuongoza. Hata Waziri Mkuu naye angeondoka, si anatoka mikoa hiyo hiyo?

  3. Sisi viongozi tunapokuwa hatutoi solution hadi tusubiri Rais au Waziri Mkuu hili linaniumiza sana. Kila mmoja atatue shida za Watanzania kwenye eneo lake kwa cheo chake"

Rais John Magufuli

Tarehe 2.7.2018 saa 10 alasiri

Unayachambuaje haya please. Dikiteita haeleweki naogopa kusema lolote!

Kazi kweli kweli Mkuu, labda tumuombe dikteta atuachambulie.

Angeongeza na Chato Airport ilijengwa na pesa ambazo hazikuidhinishwa na Bunge, ni ukiukaji wa taratibu za kuendesha Serikali

Ndege zilinunuliwa kwa pesa ambazo hazikuidhinishwa na Serikali zaidi ta Trilioni moja na ushee, ni ukiukaji wa taratibi za manunuzi ya Serikali na pia kuendesha Serikali

Kivuko cha Bagamoyo kilinunuliwa kwa shilingi bilioni 8 na kufanya kazi kwa wiki tu, ni ufosadi wa hali ya juu.

Bilioni 16 za wahanga wa tetemeko zilikwapuliwa na yours truly nao ni ufosadi na wizi wa hali ya juu.

CAG alisema 1.5 trillions hazijulikani zilipo na Wabunge wa upinzani walishinikiza iundwe tume huru kuchunguza nami nikakataa, huu ni ulevi wa madaraka.

Ongezeni Wakuu mengine mengi ambayo mtayakumbuka kuhusu huyu dhalimu.

Political cynicism inamtesa sana kitu ambacho ni kibaya sana

Usisahau kauli ya Kamanda Lissu, “Tuna Rais wa ajabu sana” mie hata kumuita Rais naona kichefu chefu.

Inapendeza sana…

Cc: @Mahondaw

In other words it is official now kuwa ccm wote lazima wasubiri jiwe awaambie kitu ili nao warudie hivyo hivyo halafu ni lazima wampigie makofi ya kumshangilia. Hakuna kutoa hoja tofauti.

Na kitendo cha kusema viongozi wasisubiri kuambiwa kina maana moja tu: kufanya anachofanya jiwe na kikubalike ambacho ni KUFANYIA WATU UKATILI NA KUVUNJA SHERIA.

JIANDAENI MLIORUDI KICHWA KICHWA JF

Kagame katuharibia mtu.

[FONT=tahoma]Tatizo ni huyo mtu anaemfundisha kuongoza nchi tawala za kidhalimu kamwe hazidumu[/FONT]

:oops::oops::oops: Ndiyo ishakuwa, huna namna mkuu…

Kuna wengine nilisikia walitaka kufanyafujo bungeni,
Nikamwambia pm,waache wafanye,Mimi nitapiga shangazi zao majimboni kwao

Dah! :oops::oops::oops: Kweli ukichaa ni mzigo mkubwa sana.

Jiwe kwenye ubora wake

Hivi kupiga huku ni kupiga kwa namna ipi? Tupate ufafanuzi wandugu maana kama mjuavyo jiwe Kiswahili kinampiga chenga si ajabu maana hii ya kupiga ina maana tofauti kabisaaaaaa :):):slight_smile:

Kauli za taahira Lusinde Bungeni dikteta ndizo anazozifagilia lakini zile za kupigania maslahi ya Watanzania hataki kabisa kuzisikia kwani mhimili wake uko juu sana ukilinganisha na mhimili wa Bunge.

https://www.youtube.com/watch?v=Zh82AC5E2kM

Fidodido Mungu anamuona

aeleze zilipo 1.5 trilion sio kufanya watu hawanamacho,lugumi vibilioni tu,yeye ni trilion yaani hata escrow haioni ndani