Makontena ya Makonda yakosa wateja

Sunday, August 26, 2018[SIZE=7] [/SIZE]

[SIZE=7]Makontena ya Makonda yakosa wateja[/SIZE]

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/4729464/highRes/2089968/-/maxw/600/-/wrqo28/-/MAKONTENA+PIC.jpg

[SIZE=5]Kwa ufupi[/SIZE]
Mizigo iliyokuwa kwenye makontena hayo inadaiwa kuwa ni samani za shule za Mkoa wa Dar es Salaam.
By Elias Msuya, Mwananchi [email protected]
Dar es Salaam. Makontena 20 yaliyo bandarini kwa jina la Paul Makonda yameshindikana kuuzwa baada ya wateja waliojitokeza kwenye mnada jana kushindwa kufika bei iliyotajwa.
Mizigo iliyokuwa kwenye makontena hayo inadaiwa kuwa ni samani za shule za Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwananchi lililofika katika mnada huo uliofanyika eneo la bandari kavu ya Malawi Cargo jana saa sita mchana lilikuta ukikaribia kufungwa na kudokezwa kuwa samani hizo zilikosa wanunuzi.
Maofisa wa TRA waliokuwepo walikataa kuzungumzia chochote.
“Kama mnataka taarifa nendeni ofisini kwa meneja wangu,” alisema ofisa wa TRA aliyekuwa akiendesha mnada huo, ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.
Hata hivyo, mmoja wa maofisa waliokuwepo katika eneo hilo alimwambia mwandishi wa habari kuwa mnada umeahirishwa kwa sababu wateja waliofika wameshindwa kufika bei iliyotakiwa.
Ofisa huyo alisema mali zilizokuwemo kwenye makontena hayo ni samani za shule.
Hata hivyo, hakutaja bei iliyokuwa inatajwa na wauzaji badala yake akamtaka mwandishi awaulize maofisa wa TRA ambao hata hivyo hawakutaka kutoa taarifa.
Baada ya kuahirisha mnada huo, msafara huo ulielekea Geti Namba 2 kufanya mnada mwingine wa magari.
Mwananchi lilidokezwa kuwa baadhi ya wamiliki na viongozi wa shule za jijini Dar es Salaam walipigiwa simu kuhusu mnada huo, lakini hawakuwa tayari kuzinunua.
Akizungumza kwa simu, Makonda, ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alisema hana taarifa ya kupigwa mnada kwa makontena hayo.
“Sina taarifa ya kupigwa mnada wa hivyo vifaa, mimi nipo msibani Mwanza, ila kauli yangu kwa walimu ambao ninawajali na kuwapenda, wasikate tamaa, nawapenda sana, ujumbe wangu mkubwa kwao ni wamtegemeao Mungu ni kama Mlima Sayuni hawatatikisika kamwe,” alisema Makonda.

Historia ya makontena
Tangazo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lililochapishwa kwenye gazeti la Serikali la Daily News Mei 12 mwaka huu, liliwataka wamiliki wa mali zilizokaa bandarini kwa zaidi ya siku 90 kujitokeza kuzilipia.
Tangazo hilo lilionyesha kuwa TRA inakusudia kufanya mnada wa wazi mwezi Juni kwa mizigo iliyokaa bandarini kwa muda mrefu bila kukombolewa, ikiwamo ya Paul Makonda.
Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa Mei 12 na Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Ben Asubisye na kuchapishwa na Daily News, wamiliki walitakiwa kuitoa mizigo hiyo ndani ya siku 30 kuanzia siku ilipotangazwa.
Katika tangazo hilo lililokuwa na orodha ya makontena zaidi ya 800, jina la Paul Makonda lilijitokeza mara 20 akiwa mpokeaji wa makontena 20 yaliyopo katika bandari kavu ya DICD yakiwa na bidhaa kadhaa kama samani.
Ingawa hakukuwa na uthibitisho kuwa Makonda ndiye mwenye makontena hayo, Februari 16 mkuu huyo wa mkoa alikaririwa katika mtandao wa gazeti la Serikali la HabariLeo kuwa alipokea makontena 20 yenye samani zitakazotumika katika ofisi za walimu zinazoendelea kujengwa. Mzigo huo ulikuwa sehemu ya shehena ya makontena 36.
Samani hizo za ofisini zilizokuwa na thamani ya Sh2 bilioni, zilitolewa na Watanzania wanaoishi Marekani wanaojulikana kama Six Region Diaspora Council.
Wakati huo, alipotafutwa na Mwananchi, mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka ilitoa notisi ya siku 30 kwa waagizaji wa mizigo ambao mizigo yao imekaa bandarini kwa zaidi ya siku 90.
“Tangazo lililotolewa ni notice (taarifa) kwa wahusika ili wakomboe mizigo yao ndani ya siku 30. Isipokombolewa itanadiwa. Mizigo hiyo inaweza kuwa ni ile ambayo haijalipiwa kodi au hata ile iliyolipiwa lakini haijaondolewa,” alisema Kayombo alipozungumza na Mwananchi, Mei 17.
Alipoulizwa kama shehena hiyo ni mali binafsi ya Makonda au ya ofisi yake, Kayombo alisema: “Majina yaliyoandikwa kwenye magazeti ndiyo taarifa za consignees (wapokeaji) zilizo kwenye nyaraka. Madhumuni ya matumizi siyo sehemu ya wajibu wetu.”
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]Baadaye, Mei 20 ilisambaa barua ya TRA, ikionyesha kuwa makontena ya Paul Makonda yana thamani ya Sh1.4 bilioni.
Barua hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilieleza kuwepo kwa ombi la msamaha wa kodi wa mali hizo kutoka kwa Makonda kwenda kwa Waziri wa Fedha, Philip Mpango, maombi ambayo hayastahili kuridhiwa, kwa mujibu wa Sheria ya Kodi.
Kadhalika, barua hiyo ambayo si Mamlaka ya Mapato (TRA) wala Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango waliothibitisha kuitambua, iliandikwa na mamlaka hiyo ya ukusanyaji kodi kumueleza waziri husika kuwa ombi hilo haliwezekani kwa kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa haina sifa ya kupata msamaha kwa mujibu wa sheria.
“Baada ya kupitia maombi hayo, tunapenda kukufahamisha kuwa sheria ya forodha ya Jumuia ya Afrika Mashariki ya 2004 na sheria ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya mwaka 2014 hazijatoa msamaha wa kulipa ushuru wa forodha na VAT kwa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa,” ilieleza barua hiyo.
Ilieleza kuwa kutokana na sheria hiyo, ofisi ya mkuu wa mkoa ni sehemu ya Serikali za Mitaa na hivyo haistahili kupata msamaha.
Barua hiyo ilitaja kiwango cha thamani ya mali hizo, ikirejea ombi la msamaha wa kodi lililowasilishwa na ofisi hiyo ya mkoa.
Kabla ya figisu hizo za msamaha wa kodi na tangazo la TRA, Februari mwaka huu, RC Makonda aliwapeleka baadhi ya walimu wa jijini Dar es Salaam, waandishi wa habari na wadau wengine kwenda bandarini ambako aliwaonyesha makontena yenye vifaa vya ofisi na vya kufundishia, akisema vimetolewa na Watanzania waishio Marekani.
Hata hivyo, vifaa hivyo ambavyo baadhi ni viti, meza na mbao za kuandikia, vilionekana ndani ya makontena vikiwa vimeshaunganishwa, tofauti na hali ya kawaida ya kusafirisha bidhaa zikiwa hazijaunganishwa ili kuziweka nyingi kwenye kontena moja kwa ajili ya nafasi.

Wizi mtupu!

Ndiyo zao hawa wahuni na mafisadi. Halafu wanazuga eti wanajenga nchi!

MAKONDA ATUA KANISANI KUZUIA MNADA WA MAKONTENA
http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2018/08/MAKONDA-1-300x300.jpg
[ul]
[li]Asema atakayenunua atalaaniwa na Mungu, arusha kombora TRA[/li][li]Ahoji jina lake, asema kama hawalipendi waliondoe kwenye makontena[/li][/ul]
Na MWANDISHI WETU, NGARA
SIKU moja baada ya makontena 20 yaliyo bandarini kwa jina la Paul Makonda, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam kufanyiwa mnada na kukosa wateja, amefanya ibada akiomba yakose wateja.
Juzi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilifanya mnada makontena hayo katika eneo la bandari kavu ya Malawi Cargo, lakini yalikosa wanunuzi baada ya waliojitokeza kushindwa kufika bei iliyotakiwa.
Jana Makonda alikwenda katika Kanisa la Anglikana wilayani Ngara, Mkoani Kagera ambako iliendeshwa ibada maalumu ya kuzuia mnada wa makotenda yenye samani za walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Makonda ambaye yupo kwenye msiba wa mama mkubwa wa mkewe, alishiriki ibada hiyo na aliwaambiwa waumini wa kanisa hilo kuwa amesali pamoja nao kwa sababu anaamini Mungu ndiye aliyempa makotenda hayo kwa ajili ya walimu wa Mkoa wake.
Alionya kuwa atakayenunua makontena hayo atalaaniwa yeye na uzao wake wote kwa sababu vya madhabahuni havichezewi.
“Nimeamua kufanya ibada hii kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwani naamini Mungu alinipa kwa ajili ya walimu wa Dar es Salaam, wanaofanya kazi katika mazingira magumu ikiwa ni jitihada zangu binafsi kuboresha mazingira yao na ni sehemu ya kumuunga mkono Rais John Magufuli.
“Rais alitambua umuhimu wa elimu na ndiyo maana kama msaidizi wake sikuona sababu ya kukaa kimya wakati mazingira ya walimu si rafiki na kusubiri kuwalaumu walimu pale watoto wanapofeli bila kufanyia kazi changamoto zao,” alisema Makonda.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kutoa elimu bure na kwamba kwa sasa kila mwezi inatumia Sh bilioni 20 kusaidia sekta ya elimu hivyo aliamua kutumia nafasi yake na uhusiano wake binafsi kusaidia juhudi hizo.
“Kama mtakumbuka nilizindua operesheni ya kuinua na kuondoa changamoto kwenye sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu na fedha hizi zilichangwa na Watanzania, kazi hii ilifanywa na Watanzania wenyewe mimi kama kiongozi nilitoa dira.
“Niliomba msaada wa vifaa kutoka kwa Watanzania waliopo nje ya nchi ili waweze kunisaidia samani za ofisi na madarasa, vifaa hivi sipeleki nyumbani kwangu, simpelekei mama yangu.
“Bali vinaenda kusaidia walimu na wanafunzi ambao wanajitolea kufanya kazi usiku na mchana katika mazingira magumu ili kuwasaidia watoto masikini.
“Cha kushangaza leo vinapigwa mnada ili kutoza kodi kwa kuwa tu makontena yameandikwa Makonda basi kama jina langu hawalipendi watafakari mzigo alionao mwalimu wa Dar es Salaam anayegombea kiti na mwanafunzi anayekaa chini.
“Inasikitisha sana leo TRA inapiga simu kuomba shule binafsi zikanunue vifaa vilivyoletwa kwa msaada na Watanzania kwa ajili ya Watanzania wenzao.
“Ninachoweza kusema tu waliopewa madaraka wawe na hofu ya Mungu, mimi sikalii viti hivyo hata kama msingi wake ni chuki mchukieni Makonda lakini si walimu,” alisema Makonda.
Alisema samani hizo za walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam zinazouzwa na TRA ikumbukwe ni msaada alioutafuta kutoka kwa Watanzania waishio Marekani ili kuboresha mazingira ya walimu.
“Watanzania waishio Marekani wakajitolea kama mchango wao kwa kampeni ya Makonda ya ujenzi wa Ofisi za Walimu, TRA imefikia uamuzi huo kwa Makonda kushindwa kulipia kodi ya Sh bilioni 1.2 kama mtu binafsi wakati furniture hizo ni msaada kwa walimu wa shule za serikali,” alisisitiza.
Akizungumza na MTANZANIA jana akiwa Wilayani Ngara, Makonda alisema amelaaniwa mtu yule atakayenunua thamani hizo za walimu.
“Kwa sababu Mungu ndiye aliyewawezesha watu wakakubali kujitolea, nakuhakikishia atakayenunua hivi vifaa vya walimu amelaaniwa yeye na uzao wake.
“Na kamwe hatafanikiwa katika maisha yake. Nayasema haya nikiwa na uhakika kwani vya madhabahuni havichezewi.
“Hili wazo la kutafuta msaada huu, aliweka Mungu ndani ya moyo wangu juu ya ujenzi wa ofisi za walimu kama sehemu ya kuboresha mazingira yao. Kwa utukufu wake Mungu akaandaa watu kuchangia tena kutoka nje na ndani ya nchi na utukufu wake umejidhihirisha.
“Kwa Watanzania kuchagia wakiwemo JKT kujitolea kujenga bure, mabenki wakanunua safuji na viwanda vimetoa mabati, nondo huku wengine wakijitolea masinki, mabomba na taa.
“Nchi ya China nao wamejenga ofisi na ndugu zetu kutoka Marekani wakaleta samani za walimu makontena zaidi ya 20. Wananchi na vyombo vya habari wakajitolea na kuendelea kuhamasisha huku walimu wakichanga kama sehemu ya kujikomboa, leo TRA wameamua kuuza samani za walimu kwa wamiliki wa kumbi za starehe ili walimu waendelee kugombania madawati na vyoo na wanafunzi .
“Mimi Paul Makonda nimefanya kwa sehemu yangu kilichobaki ni mwenye wazo atasimama siku moja kujitetea,”alisema.
Kutokaa na hali hiyo MTANZANI, ilimtafuta Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema ndiyo anarudi kutoka safarini na kwamba hajafuatilia namna mnada ulivyokwenda.
“Ndiyo narudi kutoka safarini, ngoja nifuatilie kwanza halafu nitakwambia ilivyokuwa,” alisema Kayombo.

HISTORIA YA MAKONTENA

Mei 12 mwaka huu, tangazo la TRA lilichapwa kwenye gazeti la Serikali la Daily News, likiwataka wamiliki wa mali zilizokaa bandarini kwa zaidi ya siku 90 kujitokeza kuzilipia.
Katika tangazo hilo, lililokuwa na orodha ya makontena zaidi ya 800, jina la Paul Makonda lilijitokeza mara 20 akiwa mpokeaji wa makontena 20 yaliyopo katika bandari kavu ya DICD yakiwa na bidhaa kadhaa kama samani.

Kama nauona msambwanda ulivyolowa.

Hahahahahaha

By The Citizen Reporter @TheCitizenTZ [email protected]

Dar es Salaam. Finance and Planning Minister Phillip Mpango has ordered the Tanzania Revenue Authority (TRA) to swiftly auction the 20 containers imported by Dar es Salaam Regional Commissioner Paul Makonda, a day after the RC threatened potential buyers of “a curse”.
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]
The minister, who gave the order during an impromptu visit to TRA Monday August 27, said he would not be intimidated by Mr Makonda’s threats.

On Saturday, bidders failed to reach the bidding prices of the tables, chairs and blackboards valued Sh2 billion. Mr Makonda said the furniture was meant for schools in Dar es Salaam.

The containers were put under auction after the RC failed to pay import taxes and other duties.

Speaking with The Citizen via telephone from Ngara District, Mr Makonda said he would make sure that all containers were not sold because he had asked God to block anyone attempting to buy them.
Read more: Makonda: Don’t buy containers

Hatimaye Baba AKA dikteta amsusa mwanaye.

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Ngoja tuone mwisho wa hii movie

Naam Mkuu hii vita ni kali sana maana hakuna aliyewahi kupambana na Bashite akashinda kumbuka yaliyomkuta Nape. Nyeti zinadai hata Majaliwa anamuhofia Bashite. Sasa ngoja tuone hili varangati la Mpango na bashite nani ataibuka kidedea.

https://www.youtube.com/watch?v=KQvFQBhJSm0

Waongo hawaachi asili yao! Yule muongo mwingine, “Tangu niingie madarakani 2015 nimejenga viwanda 3,060.”

Nilipoingia madarakani bei ya sukari ilikuwa Tsh.5000/- kwa kilo.

BAK1, sidhani kama amensusa! Lakini kwa upande mwingine nadhani Mpango atakuwa ameshaongea na BABAKE Bashite, hawazi kuwa na courage ya kusema aliyoyasema jana! Ngoja tusubiri!

Nasikia samani ni za hotel yake Mwanza??? Ni kweli?

Mkuu bado haijathibitika bado.maana kijana bado anaonekana kuvimba kichwa sana.

Mimi nadhani ni movie wanayotengeneza na babake ili apate kisingizio cha kumuondoa kwenye hiyo nafasi.ili amfanyie kazi ya GIZANI kwa uhuru zaidi

Kubwa la waongo hilo Mkuu.

Inawezekana ni sinema nyingine Mkuu.

Mtu asiyejulikana

Wednesday, August 29, 2018

[SIZE=7]Hatua kwa hatua sakata la makontena ya Makonda [/SIZE]

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/4734066/highRes/2093295/-/maxw/600/-/ok9bbsz/-/makonda+pic.jpg

[SIZE=5]Kwa ufupi[/SIZE]
Baada ya makontena hayo kutouzika, Jumapili Agosti 26, 2018 Makonda alitoa onyo kuwa mtu atakayenunua makontena hayo atalaaniwa
By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]
Dar es Salaam. Kitendo cha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kumshukia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu sakata la mnada wa makontena 20 yaliyopo bandarini ni kama kimerejesha upya sakata hilo lililoanza tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Makontena hayo yenye samani za kama viti, meza na mbao za kuandikia yenye umiliki wa Paul Makonda yanadaiwa kodi inayokadiriwa kuwa Sh1.2bilioni.
Jumamosi iliyopita Agosti 25, 2018 makontena hayo yalikosa wanunuzi katika mnada kutokana na watu wengi kushindwa kufikia bei iliyotajwa.
Soma Zaidi:
[U]Makontena ya Makonda yakosa wateja[/U]
Baada ya makontena hayo kutouzika, Jumapili Agosti 26, 2018 Makonda alitoa onyo kuwa mtu atakayenunua makontena hayo atalaaniwa yeye (mnunuzi) na uzao wake.
Akikagua makontena hayo Agosti 27, 2018, Waziri Mpango aliwataka viongozi serikalini kuchunguza maneno yao na akawaomba wanaotaka kununua samani hizo wasiogope.
Februari 2018
Makonda aliwapeleka baadhi ya walimu wa jijini Dar es Salaam, waandishi wa habari na wadau wengine kwenda bandarini kuwaonyesha makontena yenye vifaa vya ofisi na vya kufundisha, akisema vimetolewa na Watanzania waishio Marekani.
Hata hivyo, vifaa hivyo vilionekana ndani ya makontena vikiwa vimeshaunganishwa, tofauti na hali ya kawaida ya kusafirisha bidhaa zikiwa hazijaunganishwa ili kuziweka nyingi kwenye kontena moja kwa ajili ya nafasi.
Mei 10, 2018
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo aliieleza MCL Digital kuwa mamlaka hiyo imetoa notisi ya siku 30 kwa waagizaji wa mizigo ambayo imekaa bandarini kwa zaidi ya siku 90 kuchukua mizigo yao na kulipa stahiki zinazotakiwa.
Soma Zaidi:
[U]TRA yatishia kuuza mali za Makonda[/U]
Mei 12, 2018
Kaimu Kamishna wa Ushuru na Forodha wa TRA, Ben Asubisye alisema wamiliki wa mizigo hiyo wanatakiwa kuikomboa ndani ya siku 30 kuanzia siku hiyo.
Katika tangazo hilo lililokuwa na orodha ya makontena zaidi ya 800, jina la Paul Makonda lilijitokeza mara 20 akiwa mpokeaji wa makontena 20 yakiwa na bidhaa kadhaa zikiwemo za samani.
Mei 18, 2018
Wakati utata ukiendelea juu ya umiliki wa makontena 20 yaliyotajwa na TRA kuwa miongoni mwa yale yatakayopigwa mnada kwa kukaa bandarini muda mrefu, Makonda alisema hajui chochote na amesikia habari hizo kwenye magazeti kama walivyozisikia watu wengine.
Makonda alitoa kauli hiyo wakati akizindua kamati ya mapendekezo kuhusu wanawake waliotelekewa na wenza wao.
Sidhani kama nahusika na jambo lolote lile na sijui chochote, hilo unalolisema hata mimi nimesoma kwenye magazeti kama ulivyosoma wewe. Nafikiri zilikuwa ni habari za jana na leo nimesoma nyingine,” amesema.
[U]Makonda ayakana makontena ya Paul Makonda bandarini[/U]
Mei 20, 2018
Barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilieleza kuwa mali zilizomo ndani ya makontena 20, ambayo ni mali ya mtu anayeitwa Paul Makonda zina thamani ya Sh1.4 bilioni, ikieleza kuwepo kwa ombi la msamaha wa kodi wa mali hizo, maombi ambayo hayastahili kuridhiwa, kwa mujibu wa Sheria ya Kodi.
Kadhalika barua hiyo ambayo si TRA wala Dk Mpango waliothibitisha kuitambua, imeandikwa na mamlaka hiyo ya ukusanyaji kodi kumueleza waziri husika kuwa ombi hilo haliwezekani kwa kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa haina sifa ya kupata msamaha kwa mujibu wa sheria.
Barua hiyo ilitaja kiwango hicho cha samani ya mali hizo, ikirejea ombi la msamaha wa kodi lililowasilishwa na ofisi hiyo ya mkoa.
Soma zaidi
[U]Msimamo wa Dk Mpango dhidi ya Makonda mjadala[/U]
[U]TRA yatishia kuuza mali za Makonda[/U]