Wakati mnajisifu kuchoma nyavu za kuvulia na kupima kwa rula samaki waliovuliwa (kwa madai ya kuzuia samaki wachanga kuvuliwa) jiulizeni haya:
Kwa waliokulia au kuishi maeneo ya uvuvi; mvuvi wa dagaa huenda kuvua mahali tofauti na kutumia nyavu tofauti na mvuvi wa sato au sangara (kwa kuwa kila aina ya samaki huishi mazingira tofauti).
Sato wanaovuliwa ndani ya mipaka ya ziwa iliyopo eneo linalojulikana kwa jina Tanzania ndio hao hao sato wanaovuliwa Uganda na Kenya (wakati nyie mnazuia kuvua wenzetu wamepata fursa- sasa tutalazimika ku-import sato toka Uganda au Kenya wanaovuliwa kwenye ziwa hilo hilo moja). Sheria mliyojiwekea hata ingekuwa nzuri namna gani bado haitakuwa na manufaa kama hamtawahusisha majirani zetu.
Sato sasa hivi wanafugwa kwa mantiki hiyo si kila sato anatokea ziwa Victoria/Nyanza (na wachina walichukua mbegu ya sato na wanawafuga kwenye maji yao ambayo yapo badly polluted na wanatuletea - na mnashadidia huku watu wetu wanalishwa sato mwenye ukubwa mnaoutaka lakini wakiwa na sumu)
Dagaa hataweza kuwa na ukubwa wa sato (maana specie yake ukubwa wake ndio huo).
Sheria mliyoamua kuitekeleza itakuwa na matokeo yale yale sawa na sheria zenu nyingine: KUWAFANYA WATANZANIA WAWE MASKINI ZAIDI YA WALIVYOKUWA KABLA NYIE WA AWAMU HII HAMJAINGIZWA MADARAKANI ( NA LUBUVA NA WENZAKE WALIOKUBALI KUTUMWA WALICHOKIFANYA). MLAANIWE WAJAA LAANA NYIE
Mkuu shida ya nchi hii wanaoutunga na kusimamia sheria wao wameajiriwa na wanapata mishahara mikubwa kila mwezi achia mbali huduma nyingine bure kwa gharama ya serekali. Hizo sheria haziwaumizi kwasababu ya vipato vyao. Kibaya zaidi hawalipwi mishahara kwa ubora wa kazi zao na maamuzi yao, bali sheria za upendeleo walizojiwekea.
Watunga sera wote wa nchi hii wako Dar na hufanya kazi maofisini. Wengi wao ni wasomi wa nadharia lakini wasiojua uhalisia wa maisha ya watu wengine. Kuna waliotokea kwenye umasikini mkubwa kujisaidia haja kubwa ni porini, lakini wakipata ajira na madaraka na kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa chumbani wanajitoa ufahamu na kufanya maamuzi ya kipuuzi. Sijui kama kabla ya maamuzi yao walijiuliza waliojiajiri kwenye uvuvi wanaendeshaje maisha yao. Halafu usishangae wakitoa lugha za kejeli wakiona watu mjini kwa kusema watu hawataki kazi!
Kiongozi bora hutumia zaidi busara na hekima kuliko sheria.Muhimu zaidi ni ushawishi Wadau uvuvi,nchi washirika na elimu ya kina kwa wavuvi.Kwa ujinga na ushamba huu kuchoma nyavu za mabilioni tunaongeza umaskini,maisha duni,siha duni na chuki dhidi watawala.
Wangekua na busara wangetenga budjet ya kuhamasisha pia ufugaji wa samaki katika mabwawa au wangeaaidia wananchi kwa vikundi kuwa na zana bora za uvuvi matokeo take yangekua chanya
Halafu leo ndio anabatilisha maamuzi tena kuwa kuanzia sasa ukiwa na zaidi ya kg 20 za samaki ndio utatakiwa kuwa na kibali cha kusafirisha!!nchi kuendeshwa ki mizuka ni tabu sana!!
Sijui hii nchi wameshaiona ni ya wajinga? Kwanza ndio wanaimarisha ufisadi, hongo, NK. Hili la rula limewachafua sana. Baba akiwa hayupo mke au watoto hawawezi kubandika maharagwe mpaka baba aje apime, kama akisahau kupima asubuhi. Hittla Namba mbili kutoka Afrika.