Lusinde

ku kukikosoa chama bungeni

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akichangia
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Kwa ufupi
Ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma

By Ibrahim Yamola, Mwananchi [email protected]
Dodoma. Livingstone Lusinde amewapiga marufuku wabunge wa CCM kukikosoa chama hicho tawala ndani ya Bunge.

Mbunge huyo wa Mtera (CCM) ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Juni 25, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19, kusisitiza kuwa yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho.

“Humu ndani tunapochangia tujiepushe na kazi za wengine. Eti tukifanya hivi tutashindwa sisi si wasemaji wa chama. Sisi wabunge wa CCM kazi yetu ni kuisimamia Serikali, kukosoa na kuitetea na nasema kama bosi wenu humu ndani ni marufuku kwa mbunge wa CCM kukizungumzia chama humu,” amesema.

“Hiki ni chama chenye Serikali na tupo hapa kuisimamia si kuikosoa CCM. Chama kushinda au kushindwa si sehemu yake hapa. Kama wabunge wangu hamna lugha ya kuisifia na kuikosoa tulieni.”

Kuhusu mvutano wa korosho amesema, “Humu ndani kuna wanasheria wengi, hivi wanashindwa nini kulitolea ufafanuzi hili la korosho likaisha. Sioni haja ya kutukanana katika hili.”

tz ina wabunge vilaza

Msimlaumu hizo ni athari za kula viwavi jeshi

Halafu usikute ametumwa na mamlaka za juu, baada ya sakata la fedha za korosho…

Kwa maana hiyo atakachokiwaza Mwenyekiti hakuna wa kupinga, Nchi yetu tuna bahati mbaya sana…

Sasa mbona una mtukana wakati mwenzio kaweka bayana hoja zake? ulisha waona wana chadema wanaikosoa chadema bungeni? kosa la lusinde ni lipi? Mimi nafikiri wewe ndiye “taahira” kwa mwendo huu ikulu mtaisikia tuu kwenye bomba

Jamaa ni mpumbavu sana hajui hata wajibu wa Wabunge ni upi. Kwa akili zake finyu huyu taahira anadhani yuko Bungeni kuipigia debe Serikali na kuitetea kwenye maovu na madudu yake.

Tatizo la qualification ya Mwanasiasa ni kujua kusoma na kuandika…

Huyo Lusinde ni Std VII leaver, lakini anapewa madocuments yaliyoandikwa kiingereza na baadaye ayapitishe…

Hii TZ inarudi nyuma kwa mambo mengi sana

1.Elimu
2 Elimu
3 Elimu

SAHIHISHO: CCM ina wabunge vilaza sana

Alafu Mtu anasema kushindwa Ni moja ya sera zetu:D:D

Na wanao wachagua ndio vilaza namba moja kabisa!!

matusi yangu nawamalizia waliomchagua

Jaribu kushirikisha akili japo kwa asilimia 1

Waikosoe Chadema kwani ndiyo iliyo unda serikali? mbona wewe huwa una akili za kizoba hivi? kazi ya wabunge wanao wakilisha wananchi ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani, na kwa hilo ccm iliyo unda serikali hiyo haina pa kutokea na hata wabunge wa ccm wanayo haki ya kukosoa

Mgosi kina wengine uwasamehe fikra zimegota kwenye susu!

Hao ndio vichaa wa CCM.

Tulisema mapema binge lisiruke live…Ni gharama mmnoooo.
Sasa huu ujinga kila mmoja angejua.

Hmm! Kaazi kwelikweli…

Huyu jamaa yeye ni kuongea ujinga tu…

Mhaya umekuja kutafuta nini huku,