Lawama kwa JF na wadau wake, JF inamaana kwa Tanzania zaidi ya FB,Twitter na Instagram. malalamiko kando ya Mito ya babeli

la JF tusaidie turudi nyumbani.

ukigoogle chochote kwa lugha ya kiswahili majibu ya kwanza utayapata JF.
ukitaka msaada wa harakaharaka majibu ya haraka utayapata JF.
Ukipotea popote, ukapata majanga ukaripoti JF hata kama ni saa tisa Usiku watakuwepo wa kukusaidia.
Tofauti na FB,Twitter,Insta JF kuna moderators,content editors, wako live 24hrs/7days kumoderate mambo yasiyo sahihi kitu kinachoifanya kuwa kitu sahihi zaidi ya hizo mitandao za kighaibuni.
Habari fake, hatarishi ambazo kwa fb,instagram, twitter zinaweza kuanzishwa na kuonekana ukweli na mtu yoyote duniani JF zitafutwa, au zitakuwa Cartegorized kama TETESI na zikibainika ni chenga kutupwa na wenda muhusika kupata adhabu(BAN).
TV,RADIO na magazeti zilipata habari JF, mfano stori za kijasusi za The Bold kuandikwa magazetini, Makala za mapenzi JF kutumiwa na wakina Diva clouds, JF ilikuwa ni bomba kubwa lenye kulisha habari ghafi kwa vyanzo vingine ambavyo vilizichakata na kupata content kwenye media zao.

Habari za mange ambazo ziliandamanisha polisi nchi nzima, zilitikisa vigogo, zilisababisha press conference kila siku, zilisababisha taharuki kamwe hazikuwahi kupewa nafasi katika mtandao makini JF. Hata Salary Slip mnazi wa chadema na mpenzi wa hbr za dada huyo alipozileta ziliishia dustbin ya JF. hii ni kuonyesha umahiri wa mtandao wetu. Hapa tu nilitegemea Max apewe tuzo japo tulidukuliwa siku ya updates za maandamano kitu ambacho nilitarajia taarifa zile zingetumika kuwafuatilia waandamanaji walipo.

Ulimwengu wa mawasiliano mitandaoni umetoka enzi za mtu mmoja maarufu kuandika na wengine kupongeza na kupenda (like), bali kwenye mtu maarufu kuandika au kuongea na kuwa ameanzisha mazungumzo mitandaoni. mitandao imekaa kimazungumzo zaidi. Kwa tanzania JF pekee ndio mtandao unaotoa uhuru wa mazungumzo aina zote kuanzia pumba,udaku,siasa,ujinga,hekima,akili,maendeleo,viwanda, kilimo,biashara, utani,mapenzi, Burudani madawa na huo ndio uhalisia wa maisha mtaani.

Lawama kwa JF.
Mambo haya yamekuwepo miezi kadhaa, watu walipoanzisha thread tujadili hatma ya hizo sheria siku zikiwa halisi thread kama ziliwekwa kando, nakumbuka moja hadi jamaa akatag ID ya jamiiforum hakuna majibu. Hiki mlichokifanya kuwaacha watu kwenye mataa na kuonekana kufungia ni Surprise wataalam wanakiita WORKAROUND. mngeacha watu wajadili uhalisia wa kilichokuwa kinakuja kuwapata wenda tungepata mawazo bora zaidi. Wabunge wanaoshangaa haya leo wakati walitakiwa kushangaa wakati wa sheria zinapitishwa na kulia kwa misaada huko ulaya kama ipo ili tuwe huru nao hawafanyi vyema.

Sijui kama mkuu wetu anaogopa kukosolewa au kupingwa hadi nitakapomsikia yeye au wasaidizi wake wanasema hayo.
Sababu kubwa ni kwa sabababu hizi sheria mzizi wake ni kabla ya yeye kuja, nakumbuka nilikaa hadi usiku naangalia jinsi lissu, mnyika, makinda, mbalawa na makamba na wabunge wachache wakichuana kwa hoja katkika kupitisha sheria za mitandaoni. hiki kilichofanyika ni kuweka tofari juu ya msingi uliojengwa miaka mingi na Serikali ya chama Tawala.

Nini Kifanyike, JF wanajua wenyewe maana walikaa kimya wakati ambapo kipengele cha nini kifanyike kilipaswa kujadiliwa humohumo kabla ya tarehe 11.

Vinginevyo, Nimeikumbuka nchi yangu zayuni(jf). Nitawezaje kuimba wimbo wakati niko huku utumwani babeli?
dedication Song:By the rivers of Babylon
Bob Marley
Zaburi 137:1
By the rivers of Babylon we sat and wept
when we remembered Zion.

kama villager nimekataa kuwaza kimkumbomkumbo wa watu wa mijini

Madhara makubwa ya kuongozwa na Kichaa ndio haya…

Hata kama yeye kama hakuliasisi hili lakini yeye tayari ameshajipambanua kama mtu asiyetaka kabisa kukosolewa wala kusemwa vibaya kwenye utawala wake…

Ameshapambana na vyombo cha habari na hili limeonekana dhahiri jinsi asivyotaka kupingwa na yoyote…

Wote tunajua ni vipi Lissu alimiminiwa risasi 30 na Utawala huu…

Kufungiwa kwa JF ni sherehe kubwa kwa huyu poyoyo juha jiwe.

tujistiri tu apa kwa mdaa

kuna vitu ving sana sana vya muhm navikosa jf kupitia google asee, jf ilikua inajb maswali meng sanaa, tumetoka town tumekimbilia village, hili jukwaa ka vip tuliibe halaf tunawawekea ile notisi ya tcra nao au picha ya ubwabwa wa id, asaiv wanasherehekea idi mpaka wakishuka tupo zetu ushirombo,

Unadhani ni kwa muda gani? Mwaka mmoja? Miwili au?..

By the rivers of Babylon we sat and wept
when we remembered Zion.

kwa mujibu wa updates za page ya jf japo contents ziko kibindoni.

[I]Asante kwa kuendelea kuwa mvumilivu wakati huduma yetu ikiwa haipatikani. Tunatambua unahitaji huduma hii, tunakuhakikishia tutarejea hewani mapema iwezekanavyo!

Uongozi - JamiiForums[/I]

Hapo ndo panaponichanganya, kwangu mapema iwezekanavyo ni leoleo, kwa mwingine inaweza kuwa hata Desemba… Anyway, tuendelee kuvuta subira…

So far so good.

JF ni kama Google kwa Tanzania. Ila hawa washamba na wakwamishaji TCRA na serikali ya awamu ya 5 wameturudisha Nyuma sana. Ilivyofungwa niliwaza eti ntaanza kutegemea Radio na Tv kama sources zangu za habari!?.

Lakini jamii forums nao ni victims hapa hakuna haja ya kuwasuta na pengine hawakutaka tujadili sana sababu ishu ilikuwa mahakamani.

Tunasikikizia maumivu tu sasa ila cha muhimu ni kupata alternative itakayokuwa free forum tena kwa wabongo

Hapo ulipomalizia ndo utata ulipokuwepo sio rahisi kuruhusu mijadala kwenye kitu ambacho kipo mahakamani.

Kule jamiiforums nilikuwa nikiona post nzuri nilikuwa nasave kwenye browser.

Hii ni habari ya kutia moyo…

kinacho niuma ni taarifa na maarifa yaliyopo kwenye nyuzi mbalimbali kwenye database ya JF

Ila suluhu itapatikana tu japo hatujui ni lini. Lets keep on waiting…

Swali gumu kupata majibu ni iwapo itarudi JF yetu je content zilizokuwepo zitaendelea kuwepo maana kuna madini yalikuwa yanaitaji kuwa unarudia rudia kusoma.

Time will tell…

Cc: @Mahondaw

Hili la JF watu wanalichukulia poa,ila ni jambo la kipuuzi kuwahi kufanyika…na kama issue ni kulipia,naamini max na timu yake hawashindwi kulipia…hawa watakuwa wameshurutishwa wazime mtandao