Kwaheri wapenzi wa blog ya mashairi ya mimimalenga.

Kwanza kabisa nafuraha kubwa kujiunga na forum hii ya KenyaTalk ambayo sisiti kuita jina la ufupisho kama “KT” kama tunavyoita forum yetu ya jamiiforums kwa kifupisho cha Jf.
ni furaha kuona ndugu zetu,majirani zetu na rafiki zetu wa Kenya wamekiona kile kilichotokea kwetu nyumbani.
katika jamiiforums nilikuwa na majukwaa mengi ikiwemo jukwaa nalolipenda zaidi (jukwaa la lugha) ambalo nimekua nikiandika nyuzi mbalimbali za mashairi NA mambo ya kiswahili.
pamoja na hiyo ndugu zangu,pia nimekua ni muendesha blog (blogger) kwa muda sasa nikiendesha blog iitwayo “mimimalenga” ambayo nilianzisha kwa malengo na nia ya kuendeleza gani ya ushairi japo Mara chache sana nilipost vitu vya nje ya ushairi kwa sababu tu baadhi ya wafuatiliaji wa blog ile walikuwa wakiomba baadhi ya mambo yao kiandikwa mule.
siku chache kabla ya tangazo rasmi la serikali kutoka nilikosa nafasi ya kupost katika blog yangu kwa kuwa Ramadhani ilibana baadhi ya nyakati na hivyo kushindwa kutumia nafasi ya kuwaaga hata wapenzi wangu wa blog.
hivyo nichukue nafasi hii kuwapa shukrani na kuwaombea kila la kheri wale wote walokuwa wapo nami kwa namna mmoja ama nyingine.
muonekano mpya wa blog ya Mimi MALENGA ulifanywa na member wa jamiiforums ambae UKWELI sijawahi hata kuomuona kwa sura licha ya kufahamu tu jina lake la forum ndani ya Jf lakini alijitolea kuiweka blog KATIKA muonekano wa tofauti,sina cha kumlipa ila mungu amzidishie.
Kutokana na hali ilivyo katika suala la kusajili,gharama kuwa kubwa na sheria kuwa kama ilivyo basi sina budi kuacha kupost chochote katika blog yangu kutokana na sababu zifuatazo:
1-haikuwa blog ya kibiashara,hivyo nilikuwa siingizi chochote na sijapata chochote kutokana na blog ile ambacho kitanifanya kuifanyia usajili wa gharama kama zile.
2-nitaacha kupost ili kujiepusha na matatizo ya kisheria.
nilipenda sana mashairi yatawale katika mitandao ila basi tena,hakuna njia zaidi ya kuachana na blog na kuwaza mambo mengine.
pia niwashukuru washairi wa Kenya ambao na wao pamoja na umbali waliopo hawakusita kutuma mashairi yao katika blog yangu na yakaandikwa.
asanteni sana.
KWA HERI BLOG YA MIMI MALENGA,KWAHERI BLOG PEKEE YA MASHAIRI ILOKUWA IKIFANYA KAZI MUDA MWINGI,KWA HERI SANAA YA KISWAHILI.

Pole mkuu ndio usomaji wa namba huo tuliiambiwa na Komba ft nape nanuye

So sad daah

Inauma mkuu

Yaaani,inaumaaaaaa

Hili ndio kosa ambalo wengi hatukuliona. Unaua ubunifu bila sababu

Pole sana mkuu hii ndio Tanzania ya viwanda

So sad. Daah

Huyo bwege jiwe ata Kiswahili kinamtatiza unazani ataona manufaa ya kuwepo na blog kama yako ambayo inaendeleza Kiswahili Fasaha? Pole mkuu kama ulivyosema kuna wakenya walikua wanakutumia mashairi yao waombe wafungue Blog kutokea Kenya ili uendelee kuelimisha jamii ya wapenda kiswahili. Acha na huyo mchawi Kiswahili hajui kiingereza nacho chenga. Kumbuka maisha lazima yaende usife moyo

Hiyo sheria alie lengwa amepatikana tayari sidhan kama itazingatiwa kwa wengine

Tuliolengwa umetupata Tayri mkuu

Pole sana na hongera maana ulijitoa kuhakilisha lugha ya kiswahili inafikiwa na wengi

Waafrika ni shida sana.

Muda mwingine unaona bora Wazungu wanavyotubagua maana tutawaambukiza ujinga

Inasikitisha sana…

Cc: @Mahondaw

Pole sana, ilitakiwa mashairi ya kumtukuza mfalme tu!

Real its pain!!