Kwa wale wazoefu tupeane tips za kufanya jogging asubuhi.

Kwa wale wakongwe tuelekezane namna sahihi ya kufanya mazoezi ya kukimbia asubuhi.

Kama ;

  1. Muda wa kuamka .

  2. Uchaguzi wa raba.

  3. Muda wa kukimbia.

  4. Aina ya mazoezi ya kunyoosha viungo baada ya kumaliza kukimbia.

  5. Chakula baada ya kumaliza kukimbia.

Ninachojua tu Katika Hilo wataalam wa afya wanapendekeza muda wa kukimbia usizidi dakika 7 kwa siku.

Karibuni.

Mtu mwenye nia ya kutaka kufanya mazoezi hana muda wa kupanga hayo mambo yote, otherwise we sio mwanamazoezi ni bishoo wa mazoezi…

Kikubwa nimeona hizo dk saba kwa siku. Kwa sisi wavivu hizo dk saba hatushindwi ngoja niweke nia.

Mimi huwa nakimbia chumbani kwangu.

Duh

Unakimbiza panya?

Dk saba si akheri basi ulale na mkeo, nae atakushukuru kwa muda wako

Kwa kuanza angalau dk 20

amka saa kumi na moja Alfajili, tafuta barabara moja ndefu na changamfu, nikiwa na maana muda huo inakuwa tayari iko busy watu wanaita pita, kimbia, naamini hutokosa wenzako huko mbele, kama nia ni mazoezi, kimbia kuanzia dakika 40 mpaka Saa moja, na ukishakuwa sugu hamia ktk miinuko kidogo…hii inanikumbusha wakati nipo iringa, unashuka kile kilima cha kisima cha bibi na kukipandisha mara 20 kila asubuhi

Mi nazunguka nyumba yangu mara 30 kwa siku asubuhi na jioni

Watu wa morning glory twahitaji tizi nyingine ya ziada kweli?

ulinzi tosha huo

Tusubiri majibu

Teh teh teh…

waswahili hawachelewi kukuita mchawi:D:D:D:D

Hapana , nilijifunza kwenye ule Uzi Wa mazoezi JF sio lazima ukimbie kimbie nje hata ndani panatosha.
Ile namna ya kulala halafu miguu umeweka juu ya stuli huku ukiinua kifua nusu ni zoezi tosha lile.

Napiga kila siku asubuhi , jasho zake utadhani nimekimbia kilomita 4.

:D:D:D kabisa

  1. Amka saa 11 alfajiri
  2. Vaa raba nyepesi
  3. Vaa track suit
    4.Kimbia angalau Km 2 hadi 3 …ama kama kuna Uwanja wa Mpira wa Miguu karibu yako zunguka mara 3 - 5
  4. Piga push ups 20 hadi 50 kulingana na muda wako
  5. Fanya squats kidogo kunyosha misuli ya mapaja

Safi sana mimi huwa naruka kichurachura chumbani.