Magufuli aliingia madarakani kwa AHADI kubwa zifuatazo.
kupiga vita RUSHWA na matumizi mabaya ya madaraka.
kupiga vita uzembe na kutowajibika kwa watumishi wa uma.
kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi hasa wanyonge.
kuboresha elimu na masilahi ya wanyakazi
kuondoa UMASIKINI, MAGONJWA, UJINGA na UFISADI.
kuifanya TANZANIA YA VIWANDA.
BAADA YA TAKRIBANI MIEZI SITA TU YA UONGOZI WAKE
VITA IKABAFILIKA IKAWA DHIDI YA
kupambana na vyama vya SIASA
kuua uhuru wa vyombo vya habari
kungoa meno ya bunge
kuleta hofu kubwa ya kutekwa, kupigwa risasi nk
kuvunja katiba
kupambana na yeyote mwenye mawazo mbadala na yeye
kuigawa nchi kichama na kikanda.
KUNA MAMBO ANAFANYA VIZURI SANA LAKINI UHURU KWANGU NI MUHIMU KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE. Ndio maana tulidai UHURU wetu kutoka kwa wakoloni pamoja na kwamba walitufanyia mambo mengi.
Tabia yake bila shaka inatokana na malezi yake. Mtoto akilelewa kwenye mazingira ambayo anakosolewa vikali na kupewa adhabu nyingi kila mara mwisho wa siku anaishia kuwa mtu asiye jiamini. Akiwa mtu mzima basi hujihisi ni mtu mwenye mapungufu mengi ambayo hangependa wengine wayaone hivyo hujitahidi kuishi maisha ya kuigiza ili kuficha yale mapungufu anayohisi kuwanayo. Lakini akipata power, basi njia hubadilika na mtu wa aina hiyo hataki kusikia ukosoaji wowote ambao anaona ni kama unayaanika yale mapungufu yake. Atatumia power kuhakikisha anakua na picha safi mbele ya jamii kwa kuwapoteza wakosoaji wote. Yeye huishia kuwa dikteta
Aliingia kwa mbwembwe nyingi za nchi kujitegemea na kuwa donor country yaan waliopita wote walikuwa wanakosea na hawafai…kilichotokea ye ndio amaeirudisha nchi nyuma kwa kila kitu.
Aisee hata Mimi nafarijika sana kuwakuta huku wadai jf, hakika sasa ile atosto ya jf imepungua, tcra hawana akili maana huwezi kuziba watu midomo wasiseme, ukiwaziba lazima watafute mahala pengine pa kusemea