Huu uzi ni wangu wa pili kuhusu hili suala la kuzuri inchi jirani Tanzania. Kwa kawaida lazima nitafute ushauri na baraka za wanakijiji haswa wakati huu ninaosafiri Inchi geni. Ukitaka kuona ushauri niliopata kwa uzi wa kwanza basi fuata hii rink… http://www.kenyatalk.com/index.php?threads/kuzuru-dar.9962/ … Tarehe za kusafiri ni kama ifuatavyo
27 Dec: Nitazuru na nilale Moshi
28 Dec: Nitazuru na nilale Arusha
29 Dec: Nitazuru na nilale Dodoma
30 Dec: Nitazuru na nilale Dar es Salaam
31 Dec & 1st Jan: Nitazuru nilale siku mbili Zanzibar
2nd Jan: Nitakuwa Tanga beach: Nitafika jioni nipumzike kwa beach Kisha niamkie safari ya kurudi Mombasa
2nd Jan: Tutakuwa na @Meria Mata Mombasani…Sijui Meria kama waweza kuja Mtwapa karibu na Kendas hapo pana mpishi mzuri wa pweza…Ndoo tule pweza roast kisha ujinyunyizie chupa mbili za mvinyo kwa biri yangu.
3rd Dec: Nitarejea Nairobi.
Hii ndio safari yangu kwa google maps. Nitasafiri kwa motokaa. Mafuta yatakayotumika ni ya takriban shillingi elfu kumi na tano (Ksh 15,000 au ukipenda Tshs 131,000)
[ATTACH=full]24842[/ATTACH]
Lengo kuu la hii safari ni kujivinjari na kujiunga na watanzania kwa kuadhimisha mwaka mpya 2016. Kama uonavyo kwa ratiba niliyoichapisha, mkesha wa mwaka mpya 2016 nitakuwa Zanzibar nikifungua shampeni kwa fujo. Usiku wa tarehe mosi 2016 nitakuwa pale forodhani Zanzibar nikila pizza ya zanzibari kama uionavyo kwa hii video hapa chini.
Arusha, Babati, Kondoa, Dodoma is one long boring drive without much to see. I would do away with this section and I would rework the tour so that its Arusha, Moshi, Dar, Znz, Dar, Tanga, Mombasa… spend more time in either in Arusha, Tanga’ or Zanzibar… If you can spare some time for Pangani beach in Tanga region- the home of Baikoko
hata mimi nimepiga hesabu nikapata gari lako litakua linatumia 30 km/ltr. hapo ni ngumu mafuta utahitaji atleast 30,000 kama utatumia 15km/ltr. Na ni gari la aina gani unatumia? CC za engine ngapi?
Kwa safari kama hii ndugu yetu atahitaji gari la 2500 cc kwenda juu. Kwa mtazamo wangu pia, mafuta atahitaji takriban elfu ishirini na tano (pesa taslimu za kenya) kwenda juu
Cc Mkufuu: Ukimwona aisha umwambie nazidi kumtafuta
pengine yupo na Toyota Prius wacha atuambie lakini mkufuu usisahau picha hata kama ni ya gari kama imeisha mafuta bara barani tutashukuru. Jioni kabla ulale uweke picha ukitusimulia vile kulienda. Mimi naenda Tororo Uganda kwa motokaa hii December