Kusamehe ni dawa.

KUSAMEHE NI DAWA

Maisha ya mwanadamu siku hizi ni maisha yaliyojaa chuki na visasi Tukiishi katika maisha ya chuki na kulipizana visasi bila kusameheana basi tutazidi kusambaratika na dunia itakua siyo sehemu salama kuishi kwa kila mmoja wetu.

Msamaha ni nini?

-Msamaha ni kuondoa uchungu wote ulioumbika ndani ya moyo wako kwa hiari yako mwenyewe.

Zifuatazo ni faida za kusamehe:-

*1.Tunasamehe kwasababu kusamehe ni amri na ni agizo la Mungu Tunapaswa kusameheana kwani muasisi wa msamaha ni Mungu mwenyewe na kama Mungu angehesabu maovu yetu nani angesimama?
Anza leo kusamehe, hakuna aliye mkamilifu.Hata wewe hivyo ulivyo sio Mkamilifu

2.Tunasamehe ili tuweze kusamehewa.
Unapaswa kusamehe kwa faida yako mwenyewe siyo kwa faida ya mkosaji na wewe hebu mwachie Mungu apambane na watesi wako wala usilipe kisasi.

3.Unasamehe ili uwe na amani. Unaposamehe unakuwa unapata amani ya moyo. Mtu ambaye anavumilia uchungu ulioumbika ndani ya moyo na hataki kuachilia fundo hilo lazima litamtesa na atakosa amani ya moyo. Atahangaika na huku uchungu ulioumbika ndani ya moyo ukiendelea kumtafuta.

4.Unasamehe ili uwe na furaha. Kwa kweli ukiangalia watu wanaokataa kusameheana huwa hawana furaha kabisa katika mioyo yao. Kama unaishi katika mahusiano yoyote na mara nyingi huwa watu si wakamilifu basi msamaha ndio kiunganishi chenu ambao utarudisha uhusiano uliopotea

5.Tunasamhe ili tuwe na afya njema
Uponyaji wa kweli unaanzia moyoni. Kama mtu anasamehe kutoka moyoni basi huo ni msamaha wa kweli na ni msamaha unaoongozwa na huruma ya Mungu ndani yake. Watu hawataki kusamehe ndio maana wengine afya zao ni dhaifu. Uchungu ulioumbika ndani ya moyo unaendelaa kuwatafuna.
Usizeeke kabla ya wakati kwa ajili ya kutosamehe watu wengine

6.Kutosawasamehe watu kunakufanya ujikinai wewe mwenyewe.
Unajiona wewe ni mtu ambaye hustahili kuwepo hapa duniani. Utajiona wewe hauna maana hapa duniani utakua unakaa peke yako peke yako.
Huna furaha, amani, upendo. Maisha yako yanakuwa yamejaa sumu na majeraha moyoni ugonjwa umekuwa mkubwa na wewe hutaki kuupatia dawa ya kuuponya na dawa yake ni msamaha tu.

BARIKIWA KWA KUSAMEHEANA

Hakika mkuu mimi pia acha nipate dawa, nimewasamehe wooooote walonikosea

Ila sio alikufanya uje huku.

Nimemsamehe Jiwe

[FONT=courier new]Hayajakukuta ila nahisi Siku yakikukuta huenda Wewe ndiyo ukageuka na kuwa Rais wa Wasiosamehe duniani.[/FONT]

Tatizo binadamu ni wabishi sana…

Cc: @Mahondaw

sina kinyongo na mtu…nimesameheeeee

Ni dawa na pia ndio uhai wako binadamu,nimeipenda hii ‘Msamaha ni kuondoa uchungu wote ulioumbika ndani ya moyo wako kwa hiari yako mwenyewe’.Kusamehe kunauweka huru moyo wako na moyo ndiko zitokako chembechembe za uzima wetu,kwahiyo kama hujaachilia msamaha hakika utaingia kwenye matatizio ambayo yatakutesa wewe mwenyewe kimwili,kiafya na kiakili na hatimaye kifo chako…

sure… also forgive and forget

Kuna mtu kanifanyia jambo baya siwezi kumsamehe kwa sasa.

Nguvu ya msamaha ni kubwa mnoo,.hata kama umekosewa unaweza omba wewe msamaha…

“Unisamehe Mungu wa mbinguni kama namm nisameheavyo wengine.”

Kweli kabisa TCRA kwa hili sio wa kusameheka kabs

Wanasema ukisamehe umejitibu kidonda chako mwenyewe

Wallah tokea nimejifunza kusamehe najiona ninakua na amani kubwa moyon

Kuna mama moja alikuwa akitoa ushuda alimsamehe aliemuulia mumewe kwenye yale mauaji ya genocide ya Rwanda. Alikuwa akimpelekea msosi gerezani huu moyo wamejaaliwa wachache Mungu atusaidie tu.

Samehe 7 mara 70…

Kabisa