kurushana msuper (Hekaya)

Maboy mtaa hupigiana mabomb, kusetiana, kurushana mamanzi na visanga mob.
Paliwaga huyu msee anaitwa Exmegu. Huitwa hivo juu yee aliwaga karao masiku zake before, wakapiga mission ikabackfire akatupwa nje ya force. Saa siku hizi ni dere wa ma3 lakini aliwaga konkodi kwanza kabla apigwe jeki akawa dere.
Juzi Exmegu ametokea mtaani na tumanzi tuwili wee! Tusupuu mbaya. Si unajua tu stori za watu wa ma3? Kumendea tumanzi twa wadhii. Tumanzi tufupi alafu tumekuvalia zile mahipster za kuua mzee. Kamoja kamedandia Exmegu kwa mkono. Exmegu anajiskia ovyo. Wakaingia baesa moja ya mtaa wakapanda upstairs.
Kumbe hapa down kuna jamaa wawili wamebangaiz, wanapiga mabale zao mdogo tu. Mmoja ni Morioh na mwingine ni Kize. Morioh yuko juu ya kaveve mbaya. Taksin ni kaa ball ya golf. Ametafuna mpaka mshipa imetokea hapo juu kando ya macho ni kaa itapasuka. Wamecheki Exmegu na tumanzi, wakaangaliana wakagoteana. Baaas. Wameblow.
Morioh akaamka spidi, akaenda baesa na usuko manyu akatema ile veve, akaitisha mawoiyes. Akaosha mdomo fiti, matoothpick kwa sana. Hajui kaa huto tumanzi ni twa mtaa ama ni tumbabi. Mababi hawapendi veve.
Sasa akapanda upstairs aka kuta Exmegu saa io ndio wameletewa keroro.
Morioh, “Sasa Exmegu ni aje?
Exmegu, " Ah Morioh, vepe kaka? Si upoe down? Bamba ile seat. Salimia hawa mabeste wa mine. Huyu ni Shiroh (Saa Shiroh?), na huyu ni Wairish (Ni aje Wairish?)”. Morioh akapoa. Exmegu hajui ni kaa kuita chui kati kati ya senge.
Morioh bila kuzubaa ashawaitishia keroro ingine. Akapigia Kize mobile hapo chini, " Wee kize si ukam na hiyo drink yetu? Kuja tupoe hapa na Exmegu". Kize akapanda. Amebeba mzinga ile soo ya Viceroy. 750 mils mzee.
Wakapiga piga stori. Morioh ako na bidii ya kuitisha. Kidogo ashaitisha rao kaa tatu. Exmegu akaanza kushindwa eeh, ni aje? Hawa wasee wako na map nini? Hata tumanzi tumeanza kuskiza stori za Morioh na Kize zaidi. Na Exmegu ameanza kuskia yuko drinks kiasi.
Kidogo Morioh akachomoa bahasha akampa Wairish. Akamshow, " Hebu nishkie hii bahasha."
Wairish aka muuliza, “Ni ya?” Morioh akamshow, “Ah wee nishkie. Kuna cuzo wa mine nimeona akikam na akiniona na chapaa yee unisumbua vibaya sana”. Wairish kucheki ile burungo, imejaa machapaa. Ngiri kaa mbao na upuzi. Akasema, “Sawa, lakini usisahau”. Morioh anataka tumanzi tujue yee ana mkwanja. Actually Morioh na Kize ni mapedla wa madrugs, mataptap na mandom. Wamekungaria to death. Kutoka juu mpaka chini madesigner. Na mabling? Wachanna Prezzo.
Exmegu akaingiza njeve. Kumethoka.
Stori na rao zingine. Shiroh sasa ata ashawachilia mkono ya Exmegu. Kidogo Kize akaita Exmegu. “Na Exmegu wacha nikuulizeee, ile kisanga ulimaliza?”
“Ati?”
“Ile kisanga ya juzi tulikutoa karao”
“Wee Kize umechizi nini? Unaongea juu ya nini?”
“Wacha kujifanya Exmegu. Morioh, si huu msee tulimchangia ngiri mbao juzi atoke Buuru karao?”
Morioh akasema, “Eeeh huu chalii alipiga manzi hapa ni kaa anamada nyoka bana. Manzi akajaza P3, Exmegu ndani.”
Tumanzi tunacheki Exmegu tumepanua mdomo hatuamini.
Exmegu akasimama. Amejam vibaya mpaka mshipa ya shingo inashow. “Yaani Morioh mmekuja hapa na hio design? Wacheni wazimu! Shiroh, Wairish tuishieni wachaneni na hawa machizi!”
Tumanzi hatubanduki mzee. Tukasema na chorus, “Ah ah mi siendi!”
Mambo ya Exmegu iliishia hapo. Anyway mwishowe alichomoka akarusha mkono akawashow, “Baas, Morioh, Kize, kaeni nao! Hata kwanza ni makuro! Makuro wa mtaa hata sina haja!”
Akaishia.

13 Likes

Brathee:Dhekaya fyam lakini i sheng inaweza gashwin aende kuona mganga

5 Likes

mbona? hekaya iko tops. nimei-like sana…

3 Likes

poa sana…ingawaje ulevi inatuma nisome Mara kaa ten hivi.

2 Likes

[ATTACH=full]33767[/ATTACH]
Exmegu akicheki morioh

8 Likes

Hizi zamaanisha?
Konkodi…
Mabale…
Taksin…
Mawoiyes…
Mkwanja…
Mataptap…
Mandom…

4 Likes

Kumbe gashwin unamesea, wewe umekataa kuzeeka!

hii tuwachie gashwin ajibu

1 Like

you daring me?

1 Like

Ngweeeeeee!!!

1 Like

:D:D… nyc hekaya

1 Like

Hahah. Let Gashwin answer u that @Guru. Akilemewa nita answer

Buda Boss hiyo hekaya yako ni fyam yaani imeshika chini. tuleteage hekaya kama hizi tuchoree hizi za hawa mawerii.

1 Like

@gashwin amechukua flight hadi far east na printout ya hekaya na mkwanja ya kubribe mamorio. Lazima @Guru amtambue

5 Likes
2 Likes

konkodi- conductor
mabale- beers
taksin- fundo la miraa lililotafunwa limejazwa kwa shavu
mawoiyes- mawaba, maji
mkwanja- pesa
mataptap- matembe haramu
mandom- fangi…

ama mtasema nimemuuliza kijana wetu @Mzee mzima ?

11 Likes

Yes!:smiley: I can confirm nimepatia gashwin leakage sahii tu

10 Likes

My niece would call you guka manyanga if she was to ever see this…[ATTACH=full]33779[/ATTACH]

6 Likes

:eek::eek: Wacha aone hii, unanyimwa nunu

2 Likes

Very impressive

1 Like

Asante waniì

1 Like