Sijui kama kanjo bado wako na hii umama, I had a nasty experience ile ilifanya niwachukie hadi wa leo.
It was on a monday morning nilizindikisha mujamaa pale Machakos country bus, alikuwa anaenda gichagi. After ku bargain na kulipa fare kwa Matunda bus ikawa ni time yangu kuelekea inda mahali nilikuwa nachapa kibarua. Before kutoka hio place nikaingia kwa choo ya kanjo to empty ile uji nilikuwa nimekunywa hio morning before nitoke kejani as it was threatening to burst my bladder. Kama kawaida hio place huwa na wateja wengi so I had to wait patiently in line for my turn sahio nimekazwa yangu yote.
Kufika turn yangu nikapiga step hapo kwa urinal na kuanza kukojoa. Kabla nimalize naona kila mtu anahepa and before nishikanishe kunaendaje, huyo nikaoshwa na maji baridi iko na ile sabuni ya kuosha choo na vyenye yo hunukia vibaya, nikajikaza nakumaliza shuguli ilinipeleka hapo. Kugeuka kucheki ni aje kunaenda napata ni kamluya fulani kafupi kamevaa kabuti ya kanjo alafu kanakaa kamlevi hivi na kafegi kamejaa mate imehang kwa mdomo. Akadai ameniosha juu nakojoa kwa floor badala ya urinal na yeye ndo anaosha. Nikamuuliza kwa upole kama alikuwa amedinywa rasa hio asubuhi ama shida yake ni nini, akaanza kuongea mbaya ati ubaya ya watu wanono ni ujinga wanakuwanga wamejaza kwa kichwa. I didn’t take hio kuzoeana lightly and bila warning nikamkuta ma one two huyo chini. Nikaokota hio ndoo yake nikachota maji na kumwosha nayo alafu nikamtupia hapo chini.
Kuenda kutoka niende zangu napatana na wazito wawili kwa mlango ati mmoja wao ni supervisor, nikapigwa jeki kama ile ya makarao na hio ‘afande’ mbili nikarudishwa ndani ya choo kujibu mashtaka. Hio distance kiasi hata miguu haikugusa chini ile design nilikuwa nimebebwa juu juu, how they did it siwesjuwa. Kumbe kuna mmoja wao aliona hio action ikihappen akaenda kuitana akijua hapo lazima chai itoke. Nikaambiwa nichague moja kati ya mambo mbili. Niongee poa ama nioshe hio choo yote. Sahio ule mluya anajichocha ati lazima yeye pia anitwange juu hawes wacha tu iende hivo. Hapo nikajuwa nimepatikana juu sikuwa na chapa ingine apart from 100 bob kwa mfuko and then kuosha choo nayo, aiih! Yenyewe ukiwa umepatikana ni vizuri kutii na juu ya hio story nikakubali tu kuosha choo, sikuwa na macash za kupeana. Nikapewa equipment nianze job, nikachukua ile ndoo nilitupa down na duster bila gloves na vyenye choo ilikuwa chafu. Nikapiga survey kwanza kabla nianze hio job ndo nijue naanzia wapi sahizo majamaa wamekaa guard kwa mlango.
Nikajiambia hii ufala sifanyi so nikachora my escape plan. Nikakuta ule alikuwa anakaa mkubwa wao nikamsho enyewe leo wamenipata na nitachapa hio waks vipoa sana but na need ile kifagio ya makuti kama wako nayo ndo works ifanyike vismart. Tukaskizana anaenda kucheki kwa ka store hapo inje aniletee. Yeye kutoka tu hivi nikasho ule boy alibakia na mimi ati nafuata huyo mdosi wake nikachukue brush ya kusugua choo akaingiana box.
Nikatoka polepole na kuzunguka opposite side ya choo, nikapitia katikati ya mabasi na kuinua mdogo hivo hivo. Wale makanga na ma idlers walikuwa wana watch hio mambo walishikanisha nikuhepa nahepa wakabaki wamechangamka mbaya. I can only imagine the reaction ya huyo sos wao vyenye alirudi akaulizia ule mujamaa mnono ameenda wapi and being told by the other ‘afande’, “si alikufuata huko inje”.
Kufika hapo OTC nikadandia ma3 ya Hillock. Ma3 ikapitia hio roady hapo tu kando ya bus park nikacheki mafala bado wameshangaa nikawave na kuwaita ‘meffi nyinyi’. Nilijuwa poa jam imefunguka so hakuna vyenye wangenikuta.
Kufika kwa muhindi nayo ikawa nishachelewa and so I was not selected for kibarua for that day na hio ilimaanisha hakuna job for that whole week and so hakuna chapa ya kupepea. Ikabidi tu nirudi mtaani cursing everyone from ule mujamaa nilipeleka kwa bus, huyo mluya wa kuosha choo na mdosi wake plus huyo muhindi though yeye naye hakuwa na makosa kusema tu ukweli.