Kufunga siku ya A’shuura na siku iliyo kabla yake. A’shuura

Ni siku ya kumi katika mwezi wa Muharam (Mfungo nne).
Kwa kauli ya Mtume (saw): (Na kufunga siku ya [B]A’shuura[/B] nataraji kwa Mwenyezi Mungu kusamehewa kwa mtu madhambi ya mwaka uliyo kabla yake) [ Imepokewa na Muslim.].
Na sababu ya kufunga siku hii ni kama ilivyothibiti kutoka kwa Abdillahi ibn Abbas anasema: (Aliingia Madina Mtume (saw) akawaona Mayahudi wamefunga siku ya [B]A’shuura[/B], akasema Mtume: Ni nini hiki (mnachofanya)? Wakasema: Hii ni siku njema, siku hii ndiyo siku Mwenyezi Mungu aliyowaokoa wana israili kutokamana na maadui zao, basi akaifunga siku hii Nabii Musa. Akasema Mtume: Basi mimi nina haki zaidi kwa Musa kuliko nyinyi, akaifunga Mtume siku hiyo na akaamrisha watu kuifunga) [Imepokewa na Bukhari.].
Na inapendekezwa vile vile kufunga siku ya tisa, kwa ilivyo pokelewa kutoka kwa Mtume (saw) Alisema (Lau nitaishi mpaka Mwaka ujao nitafunga siku ya tisa) [ Imepokewa na Muslim.]
https://www.al-feqh.com/sw/saumu-funga-za-sunnah