Wakuu nawasalimia sana kutokea huku ukimbizini
Leo napenda tu kwa ufupi tutafakari namna ambavyo siasa zetu za hovyo hovyo zinavyohusika moja kwa moja na ufukara wa bara la Africa. Nchi za Africa nyingi zinaendesha siasa za “kijambazi”… yaani siasa zisizokuwa na falsafa yoyote, siasa zisizokuwa na msingi wowote, na siasa zinazotokana na mtu binafsi na zinazobadilika kulingana na nani yupo madarakani. Zaidi pia, siasa za Africa hutawaliwa na usiri mkubwa, uonevu mkubwa na kutojali kwa kwango kikubwa. Siasa za Africa pia huwa haziamini katika uweledi na ujuzi (competence) wa kitaasisi, bali huamini katika uwezo wa mtu binafsi.
Matokeo ya siasa kama hizi ni mabaya tena sana kiuchumi, na kijamii kwani hatimaye nchi husika huwa kama iko vitani (war-like economy). Kila mmoja huahangaika apate chochote, bila kujali ni halali au la. Jamii badala ya kufanya kazi, huishia kwenye struggles. Mwishowe, tija katika uchumi mpana na uchumi wa mtu mmoja mmoja huwa ya chini na hatimaye nchi huwa maskini. Nchi maskini huwa hawajilaumu wao kwamba siasa za hovyo walizo nazo ndio zinawashikilia uvunguni, bali mara nyingi huwalaumu wazungu na watu wa nje, tena kwa madhila yaliyotokea zamani kama utumwa na ukoloni.
Dawa ya kuzibadilisha nchi zetu za kiafrika wanayo waafrika wenyewe, nayo ni kuchaguwa siasa nzuri, zilizo sawia na wakati tulionao, badala ya kujificha nyuma ya vitu vya kijinga, tena viso maana.
Mfano, siasa nzuri ni ile itakayowapa wananchi fursa za elimu, ya aina yoyote kutoka mahali popote na kwa gharama yoyote. Siasa za kiafrika haziko wala karibu na swala hili kwa kuamini kuwa watu wakipata elimu itakuwa ngumu kutawaliwa. Hii ni siasa chafu kabisa
Siasa za kiafrika zimeghubikwa na usiri mkubwa tena wa kutisha. Siasa ambazo hazina falsafa, zinazoendeshwa na mtu mmoja hulazimisha watu kutohoji iwapo uelekeo ni sahihi au la. Mtu huyo mmoja kwa sababu ana madhambi yake au anatarajia kufanya madhami,;basi kwake kukosolewa ni mwiko. Hii ni siasa ya hovyo ambayo haiwezi kututoa hapa tulipo.
Siasa za kiafrika haziamini katika nguvu na vipaji vya watu mmoja mmoja katika kuzalisha mali au huduma. Badala yake, huamini kuwa mjumuisho (collectivism) unaweza kutokeza jambo zuri la maendeleo ya nchi. Siasa kama hizi ni za kivivu, tena zisizokuwa na utafiti ndani yake. Siasa kama hizi hulenga kuwafanya watu wachache kuumia wakifanya kazi huku watu wengi wakiwa hawafanyi kazi. Hili liko dhahiri katika mfumo wa kodi. Walioajiriwa kwenye mfumo rasmi ni wachache sana lakini ndo wanalipishwa kodi kuliko kundi lolote. Likija swala la upatikanaji wa huduma, hata wale wasiochangia chochote nao hutaka kunufaika sawia. Hatimaye huduma huwa mbovu kwa wote. Siasa kama hii ni ya kijinga na inakwamisha watu na jamii kuonesha uwezo wao wa mwisho katika kuzalisha mali na huduma na kukumbatia uvivu na wizi. Utakuta serikali nyingi zinaanzisha mashirika ya kibiashara tena kwa mitaji mikubwa. Bahati mbaya serikali inataka ishindane na wananchi wake kwa biashara ambazo zingefanywa makampuni ya wananchi
Siasa za Africa ni zile ambazo hazithamini ujuzi bali kufifisha ujuzi. Nchi nyingi za Kiafrika huwa zikiona kuna changamoto ambapo hazina uwezo wa kizikabili, basi hukimbilia kutunga sheria tena saa nyingine za hovyo kabisa. Mfano, mnakumbuka kipindi kile cha uchakachuaji wa disel na petrol, serikali ya TZ ilikimbilia bungeni na kupitisha sheria na bei ya mafuta ya taa ikawa sawa au zaidi ya petrol. Wananchi wengi waliumia sana lakini hawakuwa na mbadala. Mfano mwingine ni hili lisheria la maudhui ya mitandando. Serikali ya TZ ilipoona imezidiwa nguvu na mbinu za kisasa katika swala zima la teknolojia ya mawasiliano, ikaibuka na sheria, tena ya hovyo mno. Hii ni kurudisha nyuma maendeleo ya watu na nchi pia kwa kisa cha kumlinda mtu mmoja tena wa kupita tu. Mimi nafahamu sekta ya tehama imewaajiri watu wengi sana nchini Tanzania. Lakni siasa za hovyo huwa hamna kufikiria madhara ya watu kukosa ajira, achilia mbali kunyimwa haki yao ya kikatiba ya kutoa na kupokea habari.
Hizi ni baadhi siasa za hovyo kabisa ambazo Nchi za kiafrika zinapaswa zijitafakari na kuchukuwa hatuwa iwapo tunataka maendelo ya haraka na endelevu. Si ajabu ikapita miaka 100 Waafrika tukiwa katika uduni ule ule.
Karbuni tujadili