Kiswahili

@xuma Saidia.
Samefficom wanashinda wakituma huu ujumbe.
.
Sakura kwa chini ya senti 40 kwa MB kupitia kifurushi cha Safaricom cha kila siku! Bonyeza *544 chagua kifurushi cha kila siku alafu chagua 150MB +150 SMS@ SH50.
.
Swali langu ni je, kusakura ni nini?
Mimi najua kubakura
If it is what i think it is, nani walichukua hio Jina na lini?
Shukran

Sakura. Browse. Should read the entire message to get the meaning of the word.

@xuma kuja unipe 10/10

:eek:

[ATTACH=full]62732[/ATTACH]

Sakura- scratching the ground(kama kuku) looking for something to eat.

Hayo maelezo yako yanaelekeza kwenye neno ‘Chakura’

@xuma uko wapi? Njoo haraka upesi.
Sakura
Chakura
Bakura
Hebu tuelezee.
Swahili ilikuja na jahazi

Safaricom wako na ukiritimba mingi sana. Ata sijui nime sema nini but najua nime sema ni watiaji

Hapo sawa kaka.

Kwa kweli neno ‘sakura’ sijakumbana nalo katika pilkapilka zangu za uchambuzi.Lakini ukisikiliza huo ujumbe kwa ukamilifu, Safaricom wananuia kumaanisha ‘browsing’.
Ninavyofahamu, 'Browsing kwa kiswahili ni ‘vinjari’ na ‘Surfing the internet’ ni ‘kurambaza kwenye mtandao’ halafu ‘website’ ni ‘tovuti’.
Kiswahili ni lugha inayokuwa.Kwa hivyo bado tutayaona maneno mengi yakiendela kubuniwa kulingana na muktadha na mandhari ya wakati huo.Fauka ya hayo, matumizi ya maneno mapya lazima yaidhinishwe kirasmi kabla ya kutumiwa kwenye majukwaa kama yale ya kutahini.

'Kuchakura’ ni kitendo cha kukwaruza chini kutumia kucha au vidole vya mikono ukitafuta kitu kama afanyavyo kuku na vifaranga wake!

Neno sakura katika muktadha huo ni kubrowse.

Only in Ktalk “Sendro”!

Hili neno ‘Sakura’ umehakiki kwamba lipo na linatumika? Maanake nimelisaka lakini sikufanikiwa… kwa kifupi nina shaka…

:smiley: